BASI LA ISAMILO EXPRESS LAPATA AJALI MBEYA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, September 10, 2020

BASI LA ISAMILO EXPRESS LAPATA AJALI MBEYA

  Malunde       Thursday, September 10, 2020

Mnamo tarehe 10.09.2020 majira ya saa 06:40 Asubuhi huko maeneo ya Inyala – Mablock, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya – Njombe, Gari lenye namba ya usajili T.629 CQC Scania Basi mali ya Kampuni ya ISAMILO EXPRESS likitokea Mbeya kwenda Mwanza likiendeshwa na Dereva aitwaye KINI DAUD MALIMI [51] Mkazi wa Igoma Mwanza liliacha njia, kupinduka na kusababisha majeruhi na uharibifu wa Gari hilo na baadhi ya mali za abiria.

Katika ajali hiyo abiria 22 wamepata majeraha sehemu mbalimbali kati yao 12 ni wanaume na 10 ni wanawake ambapo majeruhi 08 kati yao wanaume 05 na wanawake 03 wamepelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na wengine 14 kati yao 07 ni wanaume na 07 ni wanawake wanaendelea kupatiwa matibabu Kituo cha Afya Inyala.

Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva kutaka kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari pamoja na mwendo kasi katika eneo lenye mteremko mkali.

Imetolewa na:
[ULRICH MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post