DIVA ATANGAZA KUACHA KAZI RASMI CLOUDS MEDIA


Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva the Boss ametangaza rasmi kuacha kazi katika kituo hicho baada ya kukitumikia kwa miaka 11 mfululizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diva ameandika; “Mashabiki wangu wa #AalaZaRoho mambo vipi? Mimi mwenyewe kwa akili zangu binafsi maamuzi yangu binafsi nachukua nafasi hii kuwaaga, nitawa-miss sana.

“Tumekuwa wote kwa miaka 11, worth it, natoa shukran zangu kwa uongozi wa Clouds FM kwa kunilea, Im forever thankful, shukrani kwa Joseph Kusaga na familia yake for making My Journey, ntakushukuruni sana.

“Positively nimeamua mwenyewe kuacha kazi Clouds FM leo (jana) mchana huu kwa mdomo wangu mbele ya HR na shahidi wake nilipotamka maneno hayo ya maamuzi ambayo toka natoka nyumbani nilisema nitafanya sababu ya vitu vingi tu ambavyo sitasema.

“Nashukuru sana sana sana, I’v been raised to be honest and speak up no matter what, sababu ya kusimamia ukweli wangu nimeamua fanya maamuzi ambayo nahisi ni sahihi kwangu… By saying That Life has a lot to offer Mungu yu Mwema… tutajuzana zaidi my next destination, love You all 💕,” ameandika Diva.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527