BONANZA LA MPIRA WA KIKAPU NA WAVU LAFANA KOLANDOTO

Afisa Mtendaji wa Kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga, Mwakaluba Wilson (kulia) akimkabidhi kombe la mshindi wa bonanza la mpira wa kikapu katika chuo cha sayansi za afya Kolandoto, Nahodha wa timu ya Dreamers, Salma Abdulmarick (kushoto) jana Septemba 5, 2020 chuoni hapo.

Na Mwandishi wetu - Malunde1 blog
Wanafunzi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kilichopo Manispaa ya Shinyanga, wamefanya bonanza la michezo lililojumuisha Mpira wa Wavu na Kikapu, pamoja na kupanda miche ya miti ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa manispaa hiyo kupanda miti zaidi ya Milioni 1.


Bonanza hilo lilifanyika jana (Jumamosi) katika uwanja wa mpira wa Kikapu chuoni hapo kuanzia saa 10 jioni hadi saa 3 usiku, ambapo wanafunzi pia walijumuika kupata burudani ya vinywaji na nyama choma.

Akifungua Bonanza hilo, Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Kolandoto, Mwakaluba Wilson aliahidi kuwasaidia jezi timu ya kikapu ya chuo hicho na pia kuwaunganisha ili waweze kushiriki bonanza la michezo la manispaa ya Shinyanga ambalo linatarajiwa kuunguruma mnamo Septemba 23, mwaka huu.

Wilson amewataka pia wana michezo hao hususan timu ya Kikapu kuendelea  kufanya juhudi ili wafike mbali na kuwa wachezaji wakubwa ndani na nje ya nchi.

"Lakini pia ni muhimu kuendeleza utamaduni wa mchezo huu kwa kuwarithisha wanafunzi wapya wanaoingia chuoni, ili nyinyi mtakapoondoka basi mchezo na timu yenu visife," amesema.
Mgeni Rasmi, Mwakaluba Wilson akizungumza na washiriki

Awali akisoma risala iliyoandaliwa na wachezaji wa mpira wa Kikapu, Elihu Buzuka amesema kuwa mchezo wa kikapu umekuwa moja ya michezo yenye mvuto chuoni hapo na kukitangaza chuo chao, huku akitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo Changamoto upungufu wa nyavu mbili za thamani ya Sh 20,000 na ubovu wa bodi za magoli ambazo zinahitaji kukarabatiwa ili wapate za mbao.

"Tunapungukiwa mipira (tunayo miwili tu)ambayo inamalizwa na mazingira ya kiwanja cchetu, tunaomba utusaidie kututatulia changamoto hizi na hadi sasa mabonanza matatu na tumekuwa tukiandaa michezo mbalimbali kwa gharama zetu," amesema.

Mbali na michezo, bonanza hilo lilishirikisha pia zoezi la upandaji miche ya miti 14 iliyokabidhiwa na Afisa Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga, Ezra Manjerenga ambayo ilipandwa kuzunguka uwanja wa mpira wa Kikapu chuoni hapo kwa ajili ya kumbukumbu na kuweka kivuli.

Manjerenga amesema kuwa miti hiyo ni sehemu ya mkakati wa manispaa kuhamasisha upandaji wa miti ili kufikia lengo za kupanda miti zaidi ya Milioni 1 kila mwaka.

Katika matokeo ya mchezo wa mpira wa Wavu, vijana wa Fire waliibuka na ushindi wa seti 2-1 dhidi ya Bull, huku mwisho wa mwisho na uliovuta hisia za mashabiki wengi katika bonanza hilo ulikuwa baina ya Dreamers dhidi ya Slum Dunkers, ambapo Dreamers waliibuka mabingwa wa bonanza kwa kuwachapa wapinzani wao kwa vikapu 39-37.
Mgeni rasmi wa bonanza hilo ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Kolandoto, Mwakaluba Wilson akizungumza na wanamichezo wakati wa kufungua bonanza.
Afisa Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga, Ezra Majengera akizungumza na wanamichezo kwenye bonanza hilo wakati akihamasisha zoezi la kupanda miche 14 ya miti kuzunguka uwanja wa mpira wa kikapu katika chuo cha sayansi za afya Kolandoto
Mwalimu wa mazoezi ya viungo kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, William Masala akizungumza na wana michezo kabla ya kuanza kwa bonanza hilo. 
Mmoja wa wadau wa mchezo wa kikapu, Josephine Charles ambaye pia ni Mtangazaji wa redio Faraja FM ya mjini Shinyanga, akizungumza kwenye bonanza hilo.
Afisa Mtendaji Kata ya Kolandoto, Mwakaluba Wilson akipanda mti katika eneo la uwanja wa mpira wa kikapu kwenye chuo cha afya Kolandoto

Mwakaluba akiumwagilia maji mti alioupanda
Daktari Mkuu wa hospitali ya Kolandoto, Dk. Zephania Msunza (kushoto) na Mwenyekiti wa timu ya kikapu chuoni hapo, Kibwana Mgude (kulia) wakiwa na miche ya miti tayari kutekeleza zoezi la upandaji miti chuoni hapo

Daktari Mkuu wa hospitali ya Kolandoto, Dk. Zephania Msunza akitekeleza zoezi la kupanda mche wa mti kuzunguka eneo la uwanja wa mpira wa Kikapu katika chuo cha sayansi ya afya Kolandoto
Nahodha wa timu ya mpira wa kikapu ya Dreamers ya chuo cha afya Kolandoto, Salma Abdulmarick (kulia) akiwa na mche wa mti tayari kwa kuupanda katika eneo la uwanja wa kikapu chuoni hapo
Wachezaji wa timu zote mbili za mpira wa kikapu wakifuatilia maelekezo kwa ajili ya mchezo wa bonanza hilo
Wachezaji wa Bull na Fire wakichuana kuwania mpira wakati wa mchezo wa mpira wa Wavu, ambapo Fire walishinda kwa seti 2 kwa 1
Nahodha wa timu ya mpira wa Wavu ya Fire, Ivan Charles akiruka juu kuupiga mpira wakati wa mchezo huo katika chuo cha afya Kolandoto
Wachezaji wa timu za mpira wa kikapu za Slum Dunkers na Dreamers wakigombania mpira wakati wa mchezo maalum uliowakutanisha kwenye bonanza hilo
Mchezaji wa Dreamers, Ivan Charles akimiliki mpira wakati wa mchezo wa mpira wa kikapu dhidi ya wapinzani wao, Slum Dunkers
Nahodha wa Dreamers, Salma Abdulmarick (kulia) akijaribu kuuwahi na kumdhibiti mchezaji kutoka timu pinzani wakati wa mchezo wa mpira wa kikapu ulizikutanisha timu za Dreamers na Slum Dunkers
 Mchezaji kiongozi wa Dreamers, Barnaba Johaness akitoa maelekezo kwa wenzake wakati wa mapumziko katika mchezo wa bonanza chuo cha afya Kolandoto

 Mchezaji wa Slum Dunkers, Teddy Masele (kulia) akimfukuzia mchezaji wa Dreamers kuhakikisha hapiti kuleta madhara
 Mgeni rasmi akimkabidhi kikombe cha ushindi, Nahodha wa Dreamers baada ya kuwafunga wapinzani wao Slum Dunkers vikapu 39 kwa 37
Mgeni rasmi akimvisha medali mchezaji bora wa mechi ya kikapu, Big Michael kutoka Slum Dunkers ambaye alifunga pointi 18 katika mchezo huo 
 Mgeni rasmi akimvalisha medali ya ubingwa wa mchezo wa bonanza mmoja wa wachezaji wa timu ya Dreamers
 Nahodha wa timu ya mpira wa kikapu ya chuo cha afya Kolandoto, Barnaba Johaness (kushoto) akivalishwa medali ya ubingwa baada ya timu aliyoichezea ya Dreamers kushinda mchezo maalum katika bonanza hilo

 Mwenyekiti wa timu ya mpira wa kikapu chuo cha sayansi ya afya Kolandoto, Kibwana Mgude akitoa neno la shukrani baada ya kuhitimisha bonanza
 Wachezaji wa Dreamers wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe cha ushindi 
Viongozi waliofika kushuhudia bonanza hilo wakishiriki kupiga picha na kombe

Picha zote na Damian Masyenene

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527