AMBER RUTTY, MUMEWE NA JAMES DELIOUS WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO | MALUNDE 1 BLOG

Friday, September 25, 2020

AMBER RUTTY, MUMEWE NA JAMES DELIOUS WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO

  Malunde       Friday, September 25, 2020

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’ na mpenzi wake Said Bakary na James Charles (James Delicious) kulipa faini ya Mil. 11 ama kwenda jela miaka 5 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa matatu ikiwemo kufanya mapenzi kinyume na maumbile.Hata hivyo Amberutty na wenzake wameshindwa kulipa faini hiyo kwa leo, hivyo wamepelekwa gerezani na endapo kama watalipa wataachiwa.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya baada ya mahakama hiyo kujiridhisha pasina kuacha kwa ushahidi uliotolewa na Upande wa Mashitaka.

“Nimezingatia hoja za pande zote mbili na athari za makosa haya, ni kweli washitakiwa wote vijana na wanategemewa, nimeona mshitakiwa wa kwanza anajutia

‘Mshtakiwa wa Kwanza, Pili na Tatu ni wakosaji wa kwanza, kutokana na mazingira ya kesi hii adhabu yake ni miaka 30 kila kosa ambapo nikiwafunga mtapotea kabisa

“Hivyo kwa mazingira mliyoyasema na lengo la adhabu ni kujirudi, mshitakiwa wa kwanza Utalipa Mil.3 ama jela miaka 5, mshitakiwa wa Pili utalipa faini ya Mil.3 ama jela miaka 5 na mshitakiwa wa tatu faini Mil.5 ama jela miaka 5 adhabu zitaenda sambamba” Hakimu


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post