TANESCO YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WACHIMBAJI WADOGO, VIWANDA NA MASHINE ZA KUSAGA NAFAKA


Mhandisi wa umeme kutoka TANESCO Hassan Kipende wa idara ya AMR mita akikagua miundo mbinu ya kiwanda Cha kuchakata mawe Cha even kilichoko chalinze mkoa wa Pwani.
Mashine ikichakata mawe katika kiwanda cha Even kilichoko Chalinze Mkoani Pwani.
***
Na Neema Mbuja - Kibaha

Shirika la umeme Tanzania TANESCO kupitia Idara ya masoko imeendelea na kampeni ya kutoa Elimu kwa wamiliki wa viwanda,machimbo ya madini, na mashine za kusaga kwa mkoa wa Pwani ili kuwapatia Elimu juu ya matumizi Bora ya umeme sanjari na kukagua miundo mbinu ya umeme pamoja na mota zinazotumiwa kwenye kuendesha mashine.

Miongoni mwa Elimu wanayopatiwa ni pamoja na namna ya kutumia vifaa ambavyo vinatumia umeme kidogo, umuhimu wa kukagua mota zao mara kwa mara kwa ajili ya kuleta
ufanisi na usalama wa miundo mbinu

Akizungumza na wamiliki wa viwanda kwenye Wilaya za Chalinze, Mlandizi, na Kibaha, mhandisi wa umeme kutoka idara ya AMR mita Hassan Kipende amesema kuwa kwa Sasa baadhi
ya viwanda vinatambua umuhimu wa kufunga
power factor ingawa baadhi bado hawajatambua

Kuhusu wachimbaji wadogo wa mawe eneo la Chalinze mhandisi Kipende ameshauri kuendelea kuwapatia elimu ya umuhimu wa kutumia umeme kwani wengi wao bado wanatumia
mafuta kuendesha mitambo ya kuchakata mawe jambo ambalo ni hasara kwao
Kiwanda cha kusaga nafaka cha Energy Milling kilichoko Kibaha mkoani Pwani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527