NHIF YAKANUSHA TAARIFA JUU YA KUSITISHA UTOAJI HUDUMA BAADHI YA DAWA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, September 6, 2020

NHIF YAKANUSHA TAARIFA JUU YA KUSITISHA UTOAJI HUDUMA BAADHI YA DAWA

  Malunde       Sunday, September 6, 2020
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekanusha taarifa zinazoenea kwenye Mitando ya kijamii kuwa umesitisha utoaji wa baadhi ya dawa kwa watumiaji wahuduma hiyo.


Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma Septemba 5,2020  katika ofisi za Mfuko huo Mkurugenzi Mkuu Benard Konga amesema taarifa hizo  zimeleta taharuki kwa wanachama wake

Amesema mfuko huo umejenga imani kubwa kwa wateja wake tangu kuasisiwa kwake mwaka 2001 kwa sasa una dawa 543 ambazo zikinyambulishwa zinafanya idadi ya  dawa 975  baada ya kuongeza kitita cha mafao mwaka 2016

Amewatoa hofu wanachama wa NHIF hapa nchini  na kuwataka kuendelea kutumia huduma hiyo na kutoa rai kwa wananchi kuepuka kutoa taarifa ambazo si sahihi.

Septemba 4 mwaka huu zilisambaa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mfuko wa taifa wa bima ya afya nchini(NHIF)umezifuta dawa 138 kutoka orodha ya dawa zinazotolewa na mfuko huo kwa wanachama wake.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post