MAGUFULI ASHANGAZWA MAFURIKO CCM KIRUMBA MWANZA....'NINA DENI KUBWA'

Sehemu ya Wananchi waliohudhuria Mkutano wa Kampeni za Urais za Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo tarehe 7 Septemba 2020
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM katika shamrashamra za Kampeni za Urais za CCM zilizofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 
 ****
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt John Pombe Magufuli, amesema kuwa hakutegemea kama angekutana na umati mkubwa wa watu uliojitokeza katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kusikiliza sera zake, ambapo amejiona analo deni kubwa la kufanya kazi kwa wakazi wa Jiji hilo.

Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 7, 2020, na kuwaahidi wana Mwanza wanaokaa milimani kuwa, katika kipindi kijacho hakuna mwananchi yoyote atakayebomolewa nyumba yake na huduma zote zitawafuata huko huko waliko.

"Mapokezi niliyoyapata kuanzia jana katika Mkoa huu wa Mwanza sijawahi kuyaona, sikutegemea kama Uwanja huu wa Kirumba utajaaa, wakati wa mpira watu huwa wanakaa pembeni katikati wanachezea mpira, lakini leo hata pa kuchezea mpira watu wamejaa, pembeni wamejaa na nje wamejaa", amesema Dkt Magufuli.

Akizungumzia suala la nyumba za milimani kubomolewa, Dkt Magufuli amesema, "Mwanza imebadilika sana hata hizi nyumba huko juu hazikuwepo, na katika mipango ya baadaye tunarasimisha hizo nyumba zilizopo huko juu, hakuna mtu akayebomolewa nyumba yake kule juu, Serikali itapeleka huduma zake kule kule juu, kaaeni kwa raha kwanza milimani ndiko kwenye hewa nzuri ya kuvuta".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527