Angalia Picha : MGOMBEA MWENZA URAIS CHADEMA SALUM MWALIMU AUNGURUMA NDALA - SHINYANGA MJINI


Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu akimnadi na kumuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba (kushoto).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu ameendelea na Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 za CHADEMA,ambapo leo Jumanne Septemba 22,2020 amefanya Mkutano katika kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza na Maelfu ya wananchi waliojitokea kusikiliza sera za CHADEMA,Salum Mwalimu amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 28,2020 kwenda kupiga kura na kumchagua Tundu Lissu kuwa Rais wa Tanzania, Wabunge na Madiwani ili kuwaletea maendeleo wananchi.

“Ndugu zangu naomba mjitokeze kwa wingi Oktoba 28,2020 mkachague Wagombea wa CHADEMA. Mpeni kura za kutosha Tundu Lissu,Mpeni kura za kutosha Salome Makamba kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga na hakikisheni mnachagua madiwani wote wa CHADEMA”,amesema Salum Mwalimu.

Salum Mwalimu amesema endapo CHADEMA itapata ushindi kwenye uchaguzi, watahakikisha wanaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo na ufugaji,afya,maji,umeme,biashara kwani CHADEMA inaamini katika ‘Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu’.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu akinadi sera za CHADEMA leo Jumanne Septemba 22,2020 amefanya Mkutano katika kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu akiwaombea kura wagombea wa CHADEMA.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu akizungumza na wananchi wa kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Wananchi wakifurahia jambo
Wananchi na wanachama wa CHADEMA wakisikiliza sera za CHADEMA
Wananchi na wanachama wa CHADEMA wakisikiliza sera za CHADEMA
Wananchi na wanachama wa CHADEMA wakisikiliza sera za CHADEMA
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu akiwaombea kura wagombea udiwani kupitia CHADEMA kata mbalimbali za Manispaa ya Shinyanga.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba (kushoto).
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba (CHADEMA) akiomba kura kwa wananchi achaguliwe kuwa mbunge
Wananchi na wanachama wa CHADEMA wakisikiliza sera za CHADEMA

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post