Wagombea Vyama 16 Wachukua Fomu za Urais NEC

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa fomu za uteuzi kwa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa vyama kumi na sita (16) vya siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma jana tarehe 11 Agosti 2020, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Dkt. Wilson Mahera amesema fomu kwa wagombea hao zimetolewa kuanzia tarehe 5 Agosti 2020.

Amesema kwamba wagombea hao wanatarajiwa kurejesha fomu hizo tarehe 25 Agosti 2020 kwa ajili ya uteuzi ambao utafanyika siku hiyo.

Amewataja wagombea ambao wamechukua fomu mpaka sasa kwamba ni pamoja na Seif Maalim Seif na Rashid Ligania Rai (AAFP), Philipo John Fumbo na Zaina Juma Hamisi (DP), Leopold Lucas Mahona na Khamis Ali Hassan (NRA) na John Pombe Joseph Magufuli na Samia Suluhu Hassan (CCM).

Wengine ni Muttamwega Bhatt Mgaywa na Satia Mussa Bebwa (SAU), Queen Cuthbert Sendiga na Shoka Kamis Juma (ADC), Twalib Ibrahim Kadege na Ramadhani Ali Abdallah (UPDP), Bernard Kamilius Membe na Omar Fakih Hamad (ACT Wazalendo), Cecilia Augustino Mmanga na Tabu Mussa Juma (Demokrasia Makini) na Tundu Antiphas Lissu na Salum Mwalim Juma Mwalimu (CHADEMA).

Amewataja wengine kuwa ni Hashim Rungwe Spunda na Mohammed Massoud Rashid (CHAUMMA), Khalfani Mohammed Mazrui na Mashavu Ulawi Haji (UMD), David Daud Mwaijojele na Ali Said Juma (CCK), Ibrahim Haruna Lipumba na Hamida Abdalla Huweishil na Haji Ambari Khamis (NCCR Mageuzi) na John Paul Shibuda na Hassan Kornely Kijogoo (ADA-TADEA).

Amesema kwamba chama cha NLD ambacho kilionyesha nia ya kuchukua fomu kimeiarifu tume kwamba bado hakijafanya uteuzi wa wagombea, hivyo tume itaweka utaratibu wa kutoa fomu kwa wagombea wa chama hicho watakapokuwa tayari ndani ya kipindi hiki cha utoaji wa fomu za uteuzi.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post