RC KUNENGE AFANYA ZIARA YA KUTATUA KERO ZA WANANCHI PUGU

Na Azmala Saidi - Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amefanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi Pugu Stesheni ambapo ameahidi kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hao.

Katika ziara hiyo RC Kunenge amepokea changamoto mbalimbali ikiwemo za elimu, miundombinu, maji, umeme, afya, migogoro mbalimbali na changamoto za kisheria ambapo zipo alizotatua papo kwa papo na nyingine kuzipatia utatuzi kwa kuwaelekea watendaji kuhakikisha wanazishughulikia mara moja.

Kwenye ziara hiyo RC Kunenge aliambatana na watendaji mbalimbali wa Mkoa akiwemo katibu tawala wa Mkoa, wakuu wa idara pamoja na viongozi wa Wilaya ya Ilala.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post