NEC YATOA SIKU 2 KWA VYAMA VILIVYOPATA CHANGAMOTO KUTAMBULISHA WAGOMBEA WAO BAADA YA WATU WASIOTEULIWA KUCHUKUA FOMU ZA UTEUZI


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inafuatilia zoezi la kuchukua fomu za uteuzi na kubaini kuwa kuna changamoto ambazo zimejitokeza kutokana na vyama vya siasa kutokujipanga na kuweka utaratibu mzuri wa Wagombea wao kuchukua fomu za Uteuzi.


Tume imesema kutokana na hilo watu ambao hawakuteuliwa na vyama vyao wamejitokeza na kwenda kuchukua fomu za uteuzi za kugombea Ubunge au Udiwani bila ridhaa ya vyama husika na kupelekea walioteuliwa kushindwa kuchukua fomu.

Kwa mujibu wa Tume hiyo Majimbo yaliyoathirika ni Kibamba, Mbagala, Kilombero, na Kigamboni.

Hivyo, Tume imetoa nafasi kwa vyama vya siasa kuwatambulisha Wagombea wao kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ndani ya siku 2 kuanzia Agosti 20, 2020 kwa majimbo na Kata zilizo na changamoto


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527