NEC Yafafanua Taarifa Za Wagombea Ubunge Na Udiwani Kupita Bila Kupingwa | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, August 26, 2020

NEC Yafafanua Taarifa Za Wagombea Ubunge Na Udiwani Kupita Bila Kupingwa

  Malunde       Wednesday, August 26, 2020
Tume  ya taifa ya uchaguzi (NEC) leo Agosti 26, imezungumza na wanahabari kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo uchaguzi, ambapo kubwa zaidi wametoa rai kwa vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa weledi zaidi katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Wilson Mahera amesema, hadi kufikia 6:32 mchana, tume hiyo ilikuwa haijapokea pingamizi lolote la nafasi ya urais. Mwisho wa kuweka pingamizi ni saa 10 jioni.

“Agosti 25,2020 tume ilikamilisha uteuzi wagombea urais na makamu, ubunge na udiwani, hatujatoa taarifa yoyote juu ya zoezi hili, tayari vyombo vya habari kadhaa vinaaza kutoa matokeo ya uteuzi huu, hii ni kinyume na sheria.

”Unapotangaza mtu amepita bila kupingwa hiyo inaweza pelekea uvunjifu wa amani pale mtu anapowekewa mapingamizi, isionekane ameshinda. Mimi mwenyewe mkurugenzi wa uchaguzi sijapata majina hayo rasmi.

”Kumekuwepo na dhana ambayo wanadhani watu wanakatwa, suala la uteuzi huwezi kukata mtu kwa matakwa yako, sababu tume inafanya kazi kwa kuzingatia kanuni, tumeweka masharti ya uteuzi kwa urais wa Tanzania, ubunge na udiwani.

“Unapowekea mtu pingamizi au ukiona hakuteuliwa maana yake hajatekeleza masharti, mtu akitoa maneno nje ya masharti hatafanikiwa sababau huyu akitaka rufaa atashinda. Tume inafanya kazi kwa uwazi na uhuru,” amesema Dkt. Mahera.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post