MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE WATAKAOTEULIWA NA CCM KUJULIKANA WIKI HII | MALUNDE 1 BLOG

Monday, August 17, 2020

MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE WATAKAOTEULIWA NA CCM KUJULIKANA WIKI HII

  Malunde       Monday, August 17, 2020

Majina ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakaoteuliwa kugombes ubunge kwenye Bunge la Tanzania na uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar yanatarajiwa kufahamika wiki.


CCM imetoa ratiba ya vikao vya uteuzi wa wabunge na wawakilishi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, vikao hivyo vya kuchekecha majina vinaanza leo. Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu kitaketi kesho na pia kitafanyika kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa.

Agosti 20 hadi 21 kitafanyika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Agosti 22 Jumamosi kitafanyika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post