CHADEMA YAWATAJA WARITHI WA MNYIKA NA LIJUALIKALI


Chama cha CHADEMA kimetaja awamu ya tatu ya majina ya wabunge wake watakaogombea katika Uchaguzi Mkuu ujao, wakiwemo warithi wa Jimbo la Kibamba lililokuwa likiongozwa na John Mnyika pamoja na la Kilombero lililokuwa chini ya Peter Lijualikali aliyekihama chama hicho na kwenda CCM.Majina hayo ya awamu ya tatu yamewekwa kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa chama hicho hii leo Agosti 17, 2020, ambapo chama hicho kimemteua Sina Manzi kugombea Jimbo la Temeke na Jimbo la Ilala akiteuliwa Hashim Issa.

Kwa upande wa Jimbo lililokuwa likiongozwa na John Mnyika, atakayegombea kwa mwaka huu ni Ernest Mgawe, huku Jimbo la Kilombero akiteuliwa Modestus Chitemi, Jimbo la Igunga ni Ngassa Mboje, Jimbo la Chamwino ni Samson Muhembano na Jimbo la Mchinga chama hicho kimemteua Mohamed Kamtande.

Wengine walioteuliwa hii leo ni wa Jimbo la Liwale ambaye ni Hamad Kamtande, Jimbo la Hanang na Magoma Derick Magoma, Jimbo la Kilwa Kaskazini ni Geofrey Kipengele, Jimbo la Solwa ni Mwinula Kasonzo.

Kwa upande wa John Mnyika, yeye alisema kuwa ameamua kutogombea Ubunge kwa mwaka huu na badala yake atajikita katika kujenga chama na kutumikia vyema majukumu yake ya Ukatibu Mkuu.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post