Tanzia : DR. SHIKA '900 ITAPENDEZA' AFARIKI DUNIA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, August 24, 2020

Tanzia : DR. SHIKA '900 ITAPENDEZA' AFARIKI DUNIA

  Malunde       Monday, August 24, 2020
 Dk. Shika enzi za uhai wake
Habari kutoka Hospitali ya Nyanguge Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, zimethibitisha kufariki kwa Dkt Louis Shika ambaye alijipatia umaarufu mitandaoni baada ya kutangaza kutaka kununua nyumba za mnada za Kigamboni kwa bei ya Milioni 900 au Mia tisa itapendeza zaidi.


Dr. Luis Shika maarufu kama Mzee wa 900 itapendeza amefariki Duniani jana saa nne asubuhi akiwa anauguzwa nyumbani kwa kaka yake Joseph Kidola, Wilayani Magu, Mwanza wakati wa uangalizi baada ya matibabu katika Hospitali ya Nyanguge iliyopo Magu mkoani Mwanza.

Kaka wa Marehemu amesema chanzo cha kifo cha Dr. Shika ni figo kufeli na kwamba atazikwa kesho mchana mkoani Mwanza.

 Dkt Shika alilazwa Hospitalini Nyanguge wilaya ya Magu mkoani Mwanza kwa siku kadhaa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu na umauti umemfika akiwa hospitalini hapo.

Ikumbukwe tu kipindi cha nyuma zilitoka taarifa kwamba Dkt Louis Shika anahitaji msaada wa kifenda kwa ajili ya kufanyiwa matibabu kwa sababu alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kiafya.

Awali Dr. Shika alilazwa katika Hospitali ya Bugando Mwanza ambapo alipatiwa matibabu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post