Tazama Picha : SHEREHE YA ASKARI POLISI NA WAKE ZAO ‘SHINYANGA POLICE FAMILY DAY 2020’ YAFANA..RPC AGUSA NDOA ZA ASKARI



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba (katikati) akiwa ameambatana na Maafisa wa Polisi Mkoa wa Shinyanga akiingia katika ukumbi wa Nyakahara Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuongoza Sherehe Maalumu kwa Askari polisi na familia zao ‘Shinyanga Police Family Day 2020’ kwa ajili ya kubadilishana mawazo,kunywa,kula na kupata burudani mbalimbali usiku wa Ijumaa Julai 31,2020. 



Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanya Sherehe Maalumu kwa Askari polisi na familia zao ‘Shinyanga Police Family Day 2020’ kwa ajili ya kubadilishana mawazo,kunywa,kula na kupata burudani mbalimbali.

Askari polisi na familia zao wamekutana leo Ijumaa usiku Julai 31,2020 katika ukumbi wa Nyakahara uliopo Kambaraga Mjini Shinyanga ambapo kikundi cha burudani maarufu Super Kwata CCP Police Jazz Band kutoka Shule ya Polisi Tanzania Moshi mkoani Kilimanjaro na Kambi ya Nyani kutoka Shinyanga wamekuwa kivutio kikubwa.

Akizungumza katika sherehe hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amewasihi askari polisi wa kiume kuwapenda wake zao na wake wa maaskari kuondoa mashaka kwa waume zao ili kuepuka migogoro katika ndoa zao zao.

“Niliona ni vyema leo usiku nikutane na askari polisi wa kiume na wake zao na hii imetokana na kwamba askari wa Shinyanga kwa kweli mmefanya kazi nzuri, mnafanya kazi kwa bidii,mnafanya kazi kwa uadilifu na uaminifu hadi sasa mkoa wetu ni shwari.

“Nilielekeza kila askari aje na mwenza wake kwa maana kwamba nataka kuzungumza na nyinyi. Askari wa kiume wapendeni wake zenu, naomba mjitahidi kutunza familia zenu.Askari ukitunza familia yako vizuri ikawa haina manung’uniko Mungu huweka mkono wake na familia inabarikiwa.Tujitahidi kuondoa migogoro katika ndoa”,alisema Kamanda Magiligimba.

“Lakini na nyinyi wake za askari niwaombe sana muwapende waume zenu. Kazi za polisi ni za dharura sana lakini anaporudi mme wako unakuwa na maneno mengi badala ya kumpa pole. Waombeeni waume zenu,ni vyema mme wako anapotoka nyumbani kwenda kazini piga magoti muombee arudi salama.Wake za askari wapendeni,waheshimu na muwaamini tusiwe watu wa kuwa na mashaka mashaka na waume zetu,tunajipa msongo wa mawazo”,aliongeza Kamanda Magiligimba.

Kamanda huyo wa polisi alizitaka familia za polisi zenye migogoro zifike ofisini kwake ili kutatua migogoro yao

“Mnakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu kuna askari wa kiume alijeruhiwa sehemu zake za siri na mke wake, nisingependa hili lijirudie.Lakini pia nisingependa askari wa mkoa wa Shinyanga ajiue kwa kujipiga risasi kwa sababu ya migogoro ya kifamilia. Kama kuna familia ya askari polisi ina mgogoro wowote naomba mfike ofisini tuzungumze tuondoe tofauti zenu.

“Niwaombe sana familia za askari ziwe na upendo lakini pia wake za askari ninyi kwa ninyi mpendane.Pamoja na kukutana hapa leo lakini nitatembelea wilaya zote na kukutana na wake za askari ili tuzungumze”,alisema Kamanda Magiligimba.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akiwasalimia askari polisi na wake zao katika ukumbi wa Nyakahara Mjini Shinyanga waliohudhuria kwenye Sherehe Maalumu kwa Askari polisi na familia zao ‘Shinyanga Police Family Day 2020’ kwa ajili ya kubadilishana mawazo,kunywa,kula na kupata burudani mbalimbali usiku wa Ijumaa Julai 31,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akicheza muziki na askari polisi na wake zao.
Super Kwata CCP Police Jazz Band kutoka Shule ya Polisi Tanzania Moshi mkoani Kilimanjaro wakitoa burudani.



Super Kwata CCP Police Jazz Band kutoka Shule ya Polisi Tanzania Moshi mkoani Kilimanjaro wakitoa burudani.


MC Tumaini (katikati) akicheza muziki na Vijana wa Kundi la burudani maarufu Kambi ya Nyani kutoka Shinyanga Mjini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza kwenye Sherehe Maalumu kwa Askari polisi na familia zao ‘Shinyanga Police Family Day 2020’ usiku wa Ijumaa Julai 31,2020
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza kwenye Sherehe Maalumu kwa Askari polisi na familia zao ‘Shinyanga Police Family Day 2020’ usiku wa Ijumaa Julai 31,2020
Mkuu wa Upelelezi  Mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi akizungumza kwenye Sherehe Maalumu kwa Askari polisi na familia zao ‘Shinyanga Police Family Day 2020’ usiku wa Ijumaa Julai 31,2020
Mkuu wa Upelelezi  Mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi akizungumza kwenye Sherehe Maalumu kwa Askari polisi na familia zao ‘Shinyanga Police Family Day 2020’ usiku wa Ijumaa Julai 31,2020.
Mwenyekiti wa  Kamati ya Sherehe ‘Shinyanga Police Family Day 2020’, Joseph Kiyengi akizungumza kwenye Sherehe Maalumu kwa Askari polisi na familia zao ‘Shinyanga Police Family Day 2020’ usiku wa Ijumaa Julai 31,2020
Mkuu wa Polisi wilaya ya Shinyanga akizungumza kwenye Sherehe Maalumu kwa Askari polisi na familia zao ‘Shinyanga Police Family Day 2020’ usiku wa Ijumaa Julai 31,2020



Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya  ‘Shinyanga Police Family Day 2020’ wakiwa wamebeba zawadi maalumu kwa ajili ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya  ‘Shinyanga Police Family Day 2020’, Joseph Kiyengi akielezea kuhusu zawadi mbalimbali zilizoandaliwa na kamati hiyo kwa ajili ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba.
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya  ‘Shinyanga Police Family Day 2020’ wakionesha  zawadi ya Picha iliyochorwa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba.
Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi (kulia) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Shinyanga Mjini, Grace Salia wakionesha picha iliyochorwa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akiangalia picha aliyochorwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akiangalia picha aliyochorwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha zawadi ya cheti aliyopewa na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya  ‘Shinyanga Police Family Day 2020’
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya  ‘Shinyanga Police Family Day 2020' wakimpatia zawadi ya vitenge Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akiwa amevalishwa vitenge.


Zoezi la kufungua Shampen likiendelea.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba na askari polisi wakijiandaa kugonga Cheers!!
Askari polisi na wake wa askari wakiwa ukumbini.
Cheers!
Zoezi la kugonga Cheers likiendelea
Zoezi la kugonga Cheers likiendelea


Zoezi la kugonga Cheers likiendelea
Zoezi la kugonga Cheers likiendelea
Maafisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Askari na wake wa maaskari wakiwa ukumbini.
Askari na wake wa maaskari wakiwa ukumbini.
Zoezi la kukata Ndafu likiendelea
Zoezi la kukata Ndafu likiendelea
Zoezi la kukata Ndafu likiendelea
Askari polisi na wake zao wakisubiri kulishana ndafu
Afande Joseph Kiyengi akimlisha ndafu mke wake
Zoezi la kulishana ndafu likiendelea
Mc Mama Sabuni akizungumza kwenye sherehe ya Shinyanga Police Familya Day 2020
Mc Mama Sabuni akizungumza kwenye sherehe ya Shinyanga Police Familya Day 2020.
Mc Tumaini akionesha makeke ukumbini.
Wake wa askari polisi wakicheza ukumbini
Wake wa askari polisi wakicheza ukumbini
Wake wa askari polisi wakicheza ukumbini
Wake wa askari polisi wakicheza ukumbini
Wake wa askari polisi wakicheza ukumbini
Wake wa askari polisi wakicheza ukumbini
Wake wa askari polisi wakicheza ukumbini
Wake wa askari polisi wakicheza ukumbini
Wake wa askari polisi wakicheza ukumbini
Wake wa askari polisi wakicheza ukumbini
Wake wa askari polisi wakicheza ukumbini
Wake wa askari polisi wakicheza ukumbini
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde (kulia) akimpongeza Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba kwa kazi nzuri anayofanya kuongoza jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde (kulia) akimpongeza Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba kwa kazi nzuri anayofanya kuongoza jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga.
Mwandishi wa Habari wa Star Tv, Shaban Alley akipiga picha ya kumbukumbu na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba.
Askari polisi wakipiga picha na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba 


Askari polisi wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post