DC TANO MWERA: "SERIKALI IMEPIGA HATUA KWENYE HUDUMA ZA AFYA BUSEGA"

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera

Na Mwandishi wetu - Busega

MKUU wa Wilaya ya Busega, Bi. Tano Mwera amewataka Wananchi wa Busega kutembea kifua mbele na kuendelea kuiamini Serikali yao iliyo madarakani kwani imeweza kufanya maendeleo mbalimbali na makubwa kwenye Wilaya hiyo.

Amesema hayo wakati wa kutoa ripoti maalumu ya miradi iliyotekelezwa na Serikali kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020 ndani ya Wilaya ya Busega iliyopo Mkoa wa Simiyu
ambapo Bi. Tano Mwera aliwashukuru viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine wakiwemo Makamo wa Rais, Mhe. Samia Luhuu Hassani  na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kwa uimala wao na nchi kupiga hatua.

"Viongozi wetu wameweza kuwa chachu ya kukuwa  Kitaifa na  Kimataifa kiuchumi, ulinzi na usalama, masuala ya kodi na huduma mbalimbali na tumekuwa wa mfano Afrika  na sasa tunajifunia kuwa Taifa lenye uchumi wa kati.

Chachu yao imetufanya sisi wasaidizi huku chini kusimamia vyema maagizo na miradi mbalimbali kiutekelezaji kwa mafanikio makubwa ikiwemo ya huduma za jamii, miundombinu, elimu, afya, ulinzi na usalama na mikakati ya kiuchumi kwa Wananchi na nchi kwa ujumla".Alisema.

Katika suala la Afya, Bi. Tano Mwera amesema Serikali imetoa kiasi cha Tsh. Bilioni 1.5, kwa ajili ya ujenzi wa majengo saba (7) Hospitali ya Wilaya hiyo na majengo yote yamekamilika.

"Tsh. 1.5 Bilioni fedha za Serikali imeweza kusaidia majengo muhim ya hospitali na kwa sasa yanatumika. 

Pia Serikali iliongeza kiasi cha Tsh. Milioni 300 kwa ajiri ya kukamilisha ujenzi wa jengo la wazazi (Theatre and Lanour Ward) pamoja na njia za wagonjwa  ambapo ujenzi unaendelea hivyo jumla ya fedha yote kufikia Bilioni 1.8 " Alisema.

Bi. Tano Mwera ameongeza kuwa, Upanuzi wa Vituo vya Afya vya Nassa na Igalukilo vimeweza kugharimu Tsh. 850,000,000 ambapo sasa vituo hivyo vinafanya huduma ya upasuaji kwa wananchi.

Aidha, amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendelea katika sekta ya Afya imeweza kuboresha miundombinu kwenye vituo vya afya na zahanati kwa gharama ya Tshs 606.5 Millioni.

"Serikali kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo, tumeweza kufanyia maboresho katika Zahanati za Nyamikoma, Mwasamba, Mwanhale, Ijiha, Nyaluhande, Mwamagigisi, Badugu, Ngasamo, Kalemela na vituo vya afya vya Kiloleli na Lukungu." Alisema.

Akizungumzia hali ya upatikanaji wa Dawa, Ambapo umeongezeka kwa sasa  na kufikia asilimia 95.8 2019.

Pia alisema Vifo vya kina mama wajawazito na Watoto chini ya miaka mitano vimepungua huku idadi ya kina mama waliojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya imeongezeka.

"Kwa sasa Busega huduma bora za afya zilizosimamiwa imara na serikali ya awamu ya tano zimekuwa chachu kwa Wananchi. Vifo vya uzazi vimepungua na hata idadi ya akina mama wanaenda jifungulia vituo vya afya ikiongezeka maradufu.

Haya yote ni matunda ya awamu hii ya tano lakini pia hii imefanya wananchi kupata huduma bora na hata idadi ya wananchi waliojuinga CHF iliyoboreshwa kuongezeka na imefikia 3684" aliongeza Bi. Tano Mwera.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527