PROF. ADOLF MKENDA ARUDISHA FOMU KUWANIA UBUNGE ROMBO...AJINASIBU KUFANYA SIASA ZA KISAYANSI

Joto la uchaguzi limezidi kupanda kwenye Jimbo la Rombo Mkoani Kilimanjaro,baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof Adolf Mkenda kurejesha fomu kugombea Ubunge wa Jimbo hilo huku akisindikizwa na mamia ya wakazi wa eneo hilo, huku ajinasibu kutatua kero zilizodumu kwa muda mrefu kwenye Jimbo hilo ikiwemo tatizo la maji.

Jimbo la Rombo limekuwa chini ya Chadema kwa miaka 10,ambapo Prof. Mkenda amejinasibu kufanya siasa za Kisayansi kwa ajili ya Maendeleo ya wananchi wa Rombo na siyo Siasa za porojo.
Wanachama wa CCM wakisindikiza  Prof Adolf Mkenda kurejesha fomu kugombea Ubunge wa Jimbo la Rombo
 Prof Adolf Mkenda kurejesha fomu kugombea Ubunge wa Jimbo hilo akisaini kitabu baada ya kurejesha fomu ya kugombea ubunge jimbo la Rombo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post