BONANZA LA BASKETBALL LAFANYIKA HOSPITALI YA KOLANDOTO.…JOSEPHINE CHARLES AHAMASISHA JAMII KUFANYA MAZOEZI


Mgeni Rasmi bi. Josephine Charles akiwa amenyanyua Kombe ili kukabidhi kwa Kapteni wa Timu ya Hard Target iliyoibuka na ushindi mnono.


            Na Mwandishi wetu- Malunde 1 blog 
Jamii imetakiwa kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha afya ya mwili pamoja na kujikinga na magonjwa yasiyoambukizwa.

Hayo yamesemwa na Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa Radio Faraja fm Stereo ya Shinyanga  Bi. Josepine Charles ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika Bonanza la mchezo wa Basketball uliochezwa Julai 25 2020 katika uwanja wa Michezo uliopo jirani na Hospitali ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga, uliohusisha timu nne za wanafunzi  kutoka chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Kolandoto wakiongozwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dk. Zephania Msunza na Mkuu wa Idara ya upasuaji na Usingizi Bw. Kibwana Mgude.

Josephine alisema ni vyema jamii ikajenga utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya huku akibainisha kuwa anatarajia kuona wapenzi wa mchezo wa Basketball wakiendelea kufanya mazoezi ili kuhamasisha wengine kushiriki na kujiunga na timu mbalimbali pamoja na kuandaa mabonanza mengi ili kutanua wigo wa mchezo huo kuongeza mashabiki wengi.


Ameahidi kushirikiano nao bega kwa bega kwa kila wanaloliandaa katika mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuutangaza kupitia kituo cha Radio faraja fm stereo 91.3 anachofanyia kazi lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kupenda kujihusisha na michezo mbalimbali ikiwemo Basketball ili kulinda Afya zao.

Timu zilizoshiriki katika bonanza hilo ni Dexters,Hard Target,Warriors na Los Angels ambapo Timu za Hard target na Los Angels zilifanikiwa kuingia fainali wakati zingine zikibwagwa na hatimaye Hard Target kuibuka na ushindi kwa kupata alama 19 wakati Los Angels wakipata alama  17.

Aidha wachezaji wa timu ya Hard Target walikabidhiwa Kombe pamoja na kuvishwa  medali na mgeni Rasmi,wakati huo Mfungaji bora wa magoli katika mchezo huo Bw. John Magere alivishwa medali ya kipekee na Mchezaji bora wa Bonanza hilo Bw. Geofrey Peter naye alivishwa medali ya kipekee.

Kwa upande wao waandaaji wakubwa wa Bonanza hilo ambao pia ni wachezaji wa Timu zilizoingia fainali akiwemo Mganga Mfawidhi  wa Hospitali ya Kolandoto  Dk. Zephania Msunza aliyekuwa anachezea timu ya Los Angels iliyozidiwa nguvu na timu ya Hard Target aliyokuwa anachezea Mkuu wa Idara ya Upasuaji na Usingizi Bw. Kibwana Mgude,wamemshukuru Mgeni Rasmi kwa ushirikiano wake tangu maandalizi ya bonanza hilo hadi muda wote wa mchezo huo kuanza na kumalizika na wachezaji wote pamoja na mashabiki waliofika kutazama mchezo huo na kuwataka wasikate tamaa kwani hapo ni mwanzo tu,zipo bonanza zingine zitafuata na zitakuwa na timu jirani za Basketball.


Hata hivyo baadhi ya wachezaji wa Basketball walimpongeza Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kuandaa bonanza hilo na waliahidi kucheza vizuri zaidi katika michezo itakayofuata hapo mwezi Agosti Mwaka huu.

Bonanza la Basketball lilianza majira ya saa tisa alasiri na kumalizika saa tatu usiku na kufuatiwa na hafla ya kukabidhiwa zawadi za medali na Kombe kwa wachezaji waliofanya vizuri pamoja na timu iliyoibuka na ushindi,Kunywa soda,maji kwa mishkaki na kucheza muziki kutoka kwa ma Dj wakali hadi majira ya saa tano na nusu usiku.

Tazama picha hapa chini

Baadhi ya Wachezaji wa Bonanza la Basketball wakiendelea na mchezo huo katika uwanja wa Hospital ya Kolandoto Mkoani Shinyanga. 
Mgeni Rasmi Josephine Charles  ambaye ni mtangazaji/ mwandishi wa habari Radio Faraja katikati,akiwa amesimama na wenzake wa meza kuu akiwemo Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakijiandaa kuanza kutoa Zawadi kwa Wachezaji.
Mwalimu wa Mchezo wa Bonanza Bw. Viviano Magare akitangaza washindi kwa timu na wachezaji waliocheza vizuri pamoja mfungaji Bora wa Bonanza hilo.
Mgeni Rasmi katika bonanza hilo Bi. Josephine Charles akimvisha Medali Mfungaji bora wa magoli Bw. John Magere
Mfungaji bora wa magoli Bw. John Magere akipeana mkono wa heri na mgeni rasmi Bi. Josephine Charles  ikiwa ni sehemu ya pongezi.
Mgeni Rasmi katika bonanza hilo Bi. Josephine Charles akimvisha Medali Mchezaji bora Bw. Geofrey Peter.
Mgeni Rasmi katika bonanza hilo Bi. Josephine Charles akimvisha Medali mmoja wa waandaji wakubwa wa Bonanza hilo ambaye pia ni mchezaji wa Timu ya Hard Target walioibuka kidedea Bw. Kibwana Mgude
Wachezaji wa Timu ya Los Angels wakipita mbele ya mgeni rasmi kumpa mkono japo wafarijike kwa kukosa kombe pamoja na Medali katika bonanza la Basketball.
Wachezaji wa Timu ya Los Angels wakipita mbele ya mgeni rasmi kumpa mkono japo wafarijike kwa kukosa Kombe pamoja na Medali katika bonanza la Basketball.
Wachezaji wa Timu ya Los Angels wakipita mbele ya mgeni rasmi kumpa mkono japo wafarijike kwa kukosa Kombe pamoja na Medali katika bonanza la Basketball.
Washindi wa Bonanza hilo timu ya Hard Target wakivalishwa medali na Mgeni Rasmi Bi. Josephine Charles.
Washindi wa Bonanza hilo timu ya Hard Target wakivalishwa medali na Mgeni Rasmi Bi. Josephine Charles.
Washindi wa Bonanza hilo timu ya Hard Target wakivalishwa medali na Mgeni Rasmi Bi. Josephine Charles.
Kapteni wa Timu ya Hard Target iliyoibuka na ushindi Bw. Ivan Didas akivalishwa Medali ya Kipekee na Mgeni Rasmi Bi. Josephine Charles.
Mgeni Rasmi Josephine Charles akiwa amenyanyua Kombe ili kukabidhi kwa kaptein wa Timu ya Hard Target iliyoibuka na ushindi mnono.
Kombe limekabidhiwa na Mgeni Rasmi Bi. Josephine Charles kwa Kapteni wa Timu iliyoibuka kidedea Bw. Ivan Didas katika Bonanza la Basketball.
Baadhi ya Wachezaji wakiwa katika picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi.
Baadhi ya Wachezaji wakiwa katika picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi.
Baadhi ya Wachezaji wakiwa katika picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi.
Mganga Mfawidhi wa Hosptali ya Kolandoto Zephania Msunza akiwa ameshika Kombe japo timu aliyokuwa anachezea haikuibuka na ushindi wowote licha ya kufanikiwa kushiriki Fainali.
Mtaalamu na Mkuu wa Idara ya Upasuaji na Usingizi Hospitali ya Kolandoto Bw. Kibwana Mgude. ameshika Kombe walilolichukua mara baada ya kuibuka na ushindi mnono katika timu aliyokuwa akicheza.
Mchezaji bora Bw. Geofrey Peter akiwa amenaswa na Camera wakati mchezo ukiendelea uwanjani hapo.
Wachezaji wa Timu ya Los Angels iliyozidiwa nguvu na Hard Target wakiwa katika picha ya Pamoja kabla ya kuanza mchezo wa Fainali.
Wachezaji wa Timu ya Hard Target wakiwa katika picha ya Pamoja kabla ya mchezo wa Fainali kuanza.
Kaptein wa Timu ya Hard Target Bw. Ivan Didas kushoto akiwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kolandoto Zephania Msunza.
Baadhi ya Watazamaji na mashabiki wa Mpira wa Basketball wakifuatilia kila kinachoendelea uwanjani hapo.
Washindi wa Bonanza hilo timu ya Hard Target wakiwa wamebeba Kombe lao kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa na Mgeni rasmi Josephine Charles.Picha zote na Joachim Kilolo Mwanafunzi wa Chuo cha 
Sayansi za Afya Kolandoto.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post