SHIRIKA LA BRAC TANZANIA LAIUNGA MKONO SERIKALI VITA DHIDI YA COVID 19

 Mkurugenzi wa Brac Tanzania Fordson Kafweku akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo wa vifaa kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe Dkt Fortunata Silayo


 Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Kasimu Kaoneka akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msaada huo

 Mkurugenzi wa Brac Tanzania Fordson Kafweku kushoto akimkabidhi msaada
vifaa vya kunawia mikono kwaajili ya Shule zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe,Vifaa vilivyotolewa na shirika hilo vyenye thamani ya milioni 2.2

 Mkurugenzi wa Brac Tanzania Fordson Kafweku akinawa mikono kabla ya kukabidhi  msaada vifaa vya kunawia mikono kwaajili ya Shule zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe,Vifaa vilivyotolewa na shirika hilo vyenye thamani ya milioni 2.2 kushoto ni Meneja wa Miradi wa Brac Mkoa wa Tanga Wiliam Manoah

 Sehemu ya msaada huo ambao umetolewa na Shirika la Brac wilayani Korogwe

 Sehemu ya msaada huo ambao umetolewa na Shirika la Brac wilayani Korogwe



SHIRIKA la  Brac Tanzania limeunga mkono juhudi za serikali za kupambana na ugonjwa wa Corona (Covid -19) kwa kutoa msaada wa vifaa vya kunawia mikono kwaajili ya Shule zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe.

Vifaa vilivyotolewa na shirika hilo vyenye thamani ya milioni 2.2 ni matanki kumi na mbili (12) yaliyofungwa kwenye meza maalumu pamoja na vitakasa mikono (sanitaiza) ambapo makabidhiano hayo yalifanyika kwenye ofisi za mjini Korogwe.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Brac Tanzania Fordson Kafweku alisema kwamba wameamua kutoa msaada huo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali kupambana na ugonjwa huo.

“Kwa kweli sisi kama Brac tumeguswa na jitihada za Serikali katika mapambano ya ugonjwa wa Corona (Covid - 19) tumeona ni muda muafaka kuziunga mkono kwa kutoa vifaa vya kunawia mikono katika shule”Alisema

Mkurugenzi huyo alisema kwamba msaada huo ambao wameutoa ni muendelezo wa ugawaji wa vifaa vya kunawia mikono kwaajili ya shule zilizopo katika mikoa mbalimbali hapa nchini kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kuchukua tahadhari wanapokuwa shuleni.

Awali akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe Dkt Fortunata Silayo alilishukuru shirika la Brac Tanzania kwa kuwapatia vifaa vya kunawia mikono katika shule zao ikiwa ni jitihada za kupambana na ugonjwa wa Corona (Covid - 19).

“Tunawashukuru sana Shirika la Brac kwa kuona umuhimu wa kutoa msaada huu ambao umefika wakati muafaka hivyo tunahaidi kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo”Alisema

Naye kwa upande wake Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Kasimu Kaoneka alitoa shukrani zake kwa shirika hilo huku akieleza namna watakavyotumia vifaa hivyo shuleni

Aidha alisema vifaa ambavyo wamepatiwa vitakuwa msaada mkubwa katika mapambano ya ugonjwa wa Corona (Covid – 19) ikiwemo ikiwa kama sehemu ya somo la usafisishaji wa mikono kwa wanafunzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527