RAIS MAGUFULI ATANGAZA UWANJA WA TAIFA UTAITWA UWANJA WA MKAPA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 28, 2020

RAIS MAGUFULI ATANGAZA UWANJA WA TAIFA UTAITWA UWANJA WA MKAPA

  Malunde       Tuesday, July 28, 2020

Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametangaza kubadilisha jina la Uwanja wa Taifa na kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium kama sehemu moja wapo ya kumuenzi marehemu Mkapa.

Rais amesema ameona maoni mengi ya watu kutaka uwanja huo uitwe jina la Mkapa hivyo na yeye ameridhia

“Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo,kwa sasa wengi wanataka uwanja uitwe ‘Mkapa Stadium’, Mzee Mkapa alikuwa hapendi vitu viitwe kwa jina lake, lakini kwakuwa hawezi kuniadhibu chochote amelala hapo, natamka rasmi uwanja ule uitwe Mkapa Stadium.

“Hata kwenye Michezo alitoa mchango tena nasikia alikuwa mshabiki mkubwa wa Yanga, ingawa sikuwahi kumsikia akisema hilo hadharani, Mzee Kikwete hapa ansema ni kweli kwa sababu na yeye ni Yanga, sifahamu Mzee Mwinyi yeye ni timu gani”  Amesema  Rais Magufuli


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post