MSANII MAARUFU PAPA SHIRANDULA AFARIKI DUNIA


Charles Bukeko maarufu kama 'Papa Shirandula' 

Charles Bukeko, msanii maarufu nchini Kenya aliyejulikana sana kwa jina la 'Papa Shirandula' ameaga dunia katika hospitali ya Karen mjini Nairobi 

Kulingana na msemaji wa familia Richard Ekhalie, Papa Shirandula ameaga dunia hospitali ya Karen hii leo.

Mchana huu familia ilikuwa inasubiri ripoti maalum kutoka hospitali ili kuthibitisha kilichosababisha kifo cha mpendwa wao.

Papa Shirandula alifikishwa hospitali leo asubuhi saa mbili na nusu na mke wake, akiwa hajisikii vizuri lakini wakati wanajaribu kuendelea na mchakato wa kulazwa hospitalini, Papa Sharandula akaaga dunia.

Kulingana na msemaji wa familia, Jumatano Papa Shirandula alikuwa ametoka kuandaa vipindi kama ilivyo kawaida yake lakini akawa hajisikii vizuri na kupata dawa, lakini leo usiku, hali ikawa bado inaendelea ndio mkewe akamkimbiza hospitali baada ya kuanza kusikia vibaya karibu saa kumi na moja asubuhi.

Papa Shirandula ni nani?

Charles Bukeko maarufu kama Papa Shirandula anatoka magharibi mwa Kenya eneo la Busia.

Ameacha nyuma watoto wawili na mke wake waliokuwa wanaishi mjini Nairobi.

Bukeko ambaye jina la Papa Shirandula limetokana na kipindi kimoja cha anachoshiriki kinachopeperushwa na runinga ya Citizen, amekaa katika tasnia hii ya uigizaji kwa muda sasa na ingawa msemaji wao wa familia Bwana Ekhalie hakuwa na uthibitisho wa ni lini hasa aliingia kwenye uingizaji amesema kwamba sio chini ya miaka kumi.

Mbali na kushiriki kipindi kilichompa umaarufu mkubwa, 'Papa Shirandula' ameshiriki kwenye utengenezaji wa maudhui ya kipindi hicho na kushinda Tuzo la Kalasha Award, 2010 kama muigizaji mzuri kwenye vipindi vya televisheni, pia alikuwa kwenye filamu ya 'The Captain of Nakara' mwaka 2012.

Aidha amehusika na matangazo ya biashara mbalimbali pamoja na kuendeleza kurudumu lake la uigizaji kwenye maonyesho tele aliyoshiriki katika ukumbi wa taifa wa uingizaji Kenya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527