MWANAHARAKATI WA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO MUSA NGANGALA ARUDISHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI



Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Musa Jonas Ngangala leo Julai 16,2020 amerudisha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.

Musa Jonas Ngangala alichukua fomu Julai 14,2020 na amerudisha leo kwa katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu.

Musa Jonas Ngangala ni Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto ambaye amekuwa akisaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ikiwemo vifaa vya shule,amesomesha watoto walioshindwa kuendelea na masomo ya sekondari kwa kuwapeleka vyuo vya ufundi na amewezesha vijana kujitegemea kiuchumi na vikundi 120 vya wanawake wajasiriamali katika Manispaa ya Shinyanga.

Musa Jonas Ngangala pia amewezesha ujenzi wa chumba cha kujisitiri watoto wa kike katika shule ya Sekondari Chamaguha na uanzishwaji wwa viwanda vidogo vidogo kwa kushirikiana na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) na utekelezaji wa sera za nchi katika Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu akipokea fomu ya Musa Jonas Ngangala leo Julai 16,2020 kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde blog
 Musa Jonas Ngangala akiwasili katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kurudisha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Musa Jonas Ngangala akiwasili katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kurudisha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Musa Jonas Ngangala akinawa mikono baada ya kuwasili katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kurudisha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527