MUSA NGANGALA AJITOSA KUWANIA UBUNGE SHINYANGA MJINI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 14, 2020

MUSA NGANGALA AJITOSA KUWANIA UBUNGE SHINYANGA MJINI

  Malunde       Tuesday, July 14, 2020
Musa Jonas Ngangala akionesha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
*****
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Musa Jonas Ngangala amechukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Musa Jonas amewasili katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumanne Julai 14,2020 majira ya saa tatu na kuchukua fomu ya kuomba  kugombea ubunge katika Jimbo la Shinyanga.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Musa Jonas Ngangala ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Imalilo kata ya Kitangili katika Manispaa ya Shinyanga mwenye Elimu ya Shahada ya Mipango Miji na Maendeleo amesema endapo chama chake kitampa ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini atahakikisha anasimamia na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kikamilifu ikiwa ni pamoja na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

"Nimechukua fomu ili kuomba ridhaa chama changu kinipatie nafasi ya kwenda kuwatumikia wananchi,naamini chama changu kikinipitisha kugombea Ubunge nitakuwa mwakilishi mzuri wa wananchi katika kutatua kero za wananchi na kutekeleza miradi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi",amesema Ngangala.
Musa Jonas Ngangala akinawa mikono baada ya kuwasili katika ofisi cha CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kuchukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post