SULEIMAN NCHAMBI ASHINDA KWA KISHINDO KURA ZA MAONI JIMBO LA KISHAPU


Suleimani Nchambi (kulia)
Mkutano wa Maalumu wa CCM wilaya ya Kishapu wa kupiga kura za maoni kupata mwanachama wa CCM atakayegombea Ubunge Jimbo la Kishapu katika uchaguzi Mkuu mwaka 2020 uliofanyika Jumatatu Julai 20, 2020 umemalizika  Julai 21,2020 saa saba usiku ambapo Suleiman Nchambi aliyekuwa anatetea kiti chake ameshinda kwa kishindo katika uchaguzi huo kwa kupata kura  544 akifuatiwa na  Kishiwa Francis Kapale aliyepata kura 54 na Boniphace Butondo kura 40.

Jumla wajumbe waliotakiwa kupiga kura ni 934, wajumbe waliowapiga kura ni 882, zilizoharibika 2.
Suleimani Nchambi akiwa amebeba kura zake
Suleimani Nchambi akisaini matokeo ya uchaguzi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post