MKUU WA WILAYA MPYA WA MVOMERO ANZAA KAZI RASMI AWAONYA WAZEMBE KATIKA WILAYA HIYO

Mkuu Wilaya ya Mvomero Albinus Mgonya akipokea taarifa kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mohammed Utali wakati wa makabidhiano ya ofisi hiyo
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Mvomero Mwl Mohammed Utali akiwasilisha taarifa kwa wadau mbalimbali waliohudhuria zoezi za makabidhiano ya ofisi
Mkuu wa Wilaya Mvomero Albinus akielezea mikakati yake katika KIkao hicho cha Makabidhiano ya ofsi
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Albinus Mgonya akiagana na aliyekuwa mkuu wa Wila hiyo Alhaj Mwalim Mohameed Utali

WATENDAJI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro wametakiwa kufanya kazi kwa umoja ili kuhakisha wanafikia malengo yalikusudiwa na serikali ikiwemo kutoa huduma bora kwa wananchi.

Wito huo umetolewa na Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Mvomero Mkoani Morogoro Mwalimu Mohammed wakati wa zoezi la makabidhiano ya ofisi na Mkuu wa Wilaya Mpya wa Mvomero Albinus Mgonya.

Mwalim Utali Amesema kuwa njia ya kuweza kufika mafanikio ni kuweza kuwa kitu kimoja na kuepukana na makundi ambayo yataleta majungu hali ambayo itasababisha kutotolewa kwa huduma bora kwa wananchi.

Aidha amempongeza Mkuu wa huyo wa Wilaya ya Mvomero aliyeteuliwa hivi karibuni ambae alikuwa katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Rukwa na Kumataka kufanya kazi zake kwa uadilifu kikiwa ni pamoja na kuitumia vyema kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo katika kukabiliana na Migogoro

Hata hivyo Mwalimu Utali amesema kuwa hivi sasa wamefanikiwa kudhibiti migogoro baina ya wakulima na wafugaji tofauti na hapo awali,huku pia miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikitekelezwa.

Nae Mkuu wa Wilaya Mpya wa Mvomero Albinus Mgonya amesema kuwa atahakikisha anashirikiana vyema na watendaji wa wilaya hiyo huku pia akizingatia kiapo cha maadili katika kuwatumikia wananchi wa wilaya hiyo.

Sanjari na hilo Mgonya amesema kuwa Wilaya hiyo itakuwa na vipaumbele saba akiwemo ukusanyaji wa mapato na kukabialiana na madawa ya kulevya hasa kilimo cha Bangi,na matumizi ya ardhi ili kuepukana na migogoro

Amesema hatakuwa na huruma kwa watumishi wa Wilaya hiyo watakaobainika kuhujumu mapato ya Halmashuri ikiwemo kutoyawasilisha benki licha ya kuwa wameyakusanya kutoka kwa wananchi.

Katika Hatua nyingine amesema kuwa atakikisha anasimamia miradi ili itekelezwe kwa mujibu wa ratiba pamoja na kiwango ili iendane na thamani hali ya pesa inayotolewa na serikali

Ameeleza kuwa atahakikisha anatenga siku tatu kwa wiki kwaajili ya kwenda katika maeneo mbalimbali ya wananchi na hatokuwa Mkuu wa Wilaya wa kukaa ofisini pekee yake.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Albinus Mgonya amesema kuwa ili kuhakisha kazi zinafanyika kwa ufanisi katika ziara zake kwa baadhi ya maeneo atakuwa anakwenda bila kutoa taarifa hasa maeneo ya shule ili kuangalia maudhurio ya walimu kama wameingia kwa wakati pamoja mipango kazi yao.

Sanjari na hayo Mkuu wa Wilaya ya Mvomero amekutana na kufanya mazungumzo na watendaji katika wilaya hiyo na kuwataka kufanya kazi zao kwa ufanisi na hawatokuwa tayari kumvumilia yeyote ambae atakuwa chanzo cha kukwamisha maendeleo ya wilaya hiyo

Nae Mkurugenzi wa Wilaya Mvomero Hassan Njama amesema kuwa atakuwa tayari kukosolewa pale anakosea lengo lilikiwa ni kuhakikisha huduma bora inatolewa sambamba na kuharakisha maendeleo ya Wilaya hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527