WANANCHI KATA YA PUMA MKOANI SINGIDA WATENGENEZA MADAWATI YENYE THAMANI YA SH. MILIONI 3.4

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Mika Likapakapa (kulia mwenye baraghashia) akikabidhi jana moja ya dawati kati ya 71 kwa Wazazi wa Kata ya Puma yaliyotengenezwa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya kukaa chini kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma. 

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Mika Likapakapa, akiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Msingi Puma baada ya kukabidhi madawati hayo.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi madawati hayo.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Mika Likapakapa (katikati) , akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma baada ya kukabidhi madawati hayo.


Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma wakiwa wamekaa kwenye  madawati hayo baada ya kukabidhiwa. 
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi madawati hayo.
 Viongozi wakiwa meza kuu kwenye hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya  Shule ya Msingi Puma, Joseph Helman akizunguma kwenye hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Puma, Samuel Mdimi akizunguma kwenye hafla hiyo.
 Afisa Utamaduni wa wilaya hiyo, Abubakar Kisuda akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Puma, Wenseslaus Masire  akizunguma kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu iliyosimamia kutengeneza madawati hayo, Clemence Mande,  akizunguma kwenye hafla hiyo.

 Katibu wa Kamati ya hutengenezaji wa madawati hayo, Samsoni Masasi, akisoma taarifa.
 Wananchi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wajumbe wa Kamati Maalumu ya Kutengeneza madawati hayo wakitambulishwa.
Mwalimu, Christina Lyimo,  akizungumzia msaada wa madawati hayo.

 Mkazi wa Puma, Magreth Agustino, akizungumzia msaada wa madawati hayo.
Mwanafunzi Mariam Abdallah akizungumzia msaada wa madawati hayo.


Na Dotto Mwaibale, Singida

WANANCHI wa Kata ya Puma wilayani Ikungi mkoani Singida kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamefanikiwa kutengeneza madawati 71 yenye thamani ya sh.3,408,000 kwa ajili ya kupunguza changamoto ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma ya kukaa chini.

Hatua ya kutengeneza madawati hayo  ni kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari na kusoma katika mazingira bora.

Akizungumza jana wakati akipokea madawati hayo kutoka kwa kamati maalumu iliyosimamia hutengenezaji wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa aliipongeza kamati hiyo, wananchi na viongozi mbalimbali kwa kufanikisha kazi hiyo.

Alisema kazi walioifanya ni kubwa mno na italeta faraja kwa wanafunzi baada ya kupata madawati hayo.

"Mimi kama kiongozi mkuu niliye ndani ya Wilaya ya Ikungi ninaye isimamia Serikali kwa hawa walioshiriki kufanya kazi hii tutawatambua kwa kuwapa vyeti vya utambuzi wa kazi hiyo jambo litakalo wasaidia kuwatia moyo" alisema Likapakapa.

Alisema katika utekelezaji wa kazi hiyo anajua walikumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo za watu waliotoa ahadi kushindwa  kutoa fedha hizo ingawa watoto wao wapo shuleni hapo na watakaliaa madawati hayo.

Likapakapa alitumia mkutano huo kutoa sh.100,000 kama mchango wake wa kuunga mkono jitihada za wananchi hao katika shughuli za maendeleo.

Afisa Utamaduni wa wilaya hiyo, Abubakar Kisuda akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Justice Kijazi aliwashukuru wananchi hao kwa kazi hiyo ya kujitolea kwa moyo wa dhati na kuwa wazalendo.

Kisuda alisema mwaka 2015 katika utekelezaji wa ilani ya CCM wilaya hiyo ilitarajia kutengeneza madawati 5000 katika kipindi chote cha miaka mitano lakini hadi sasa wana asilimia 75 ya madawati yote waliyokusudia kuyatengeneza na ili kukamilisha mchakato wa kuyatengeneza ilihitajika nguvu kutoka kwa wananchi pamoja na wadau. 

"Puma imekuwa ni kijiji cha nne kati ya vijiji vilivyoweka jitihada za kutatua changamoto hii ya kutengeneza madawati." alisema Kisuda.

Alivitaja vijiji hivyo kuwa ni Unyahati, Nkhoire, Kisuluda na Puma na kuwa wazazi wote waliochangia kutengeneza madawati hayo wametimiza wajibu wao na wanakila sababu ya kupongezwa.

Kisuda alisema kwa muitikio huo waliouonesha halmashauri hiyo inawaahidi kuwapa kipaumbele katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye shule hiyo kama walivyofanya mradi wa choo ambapo kuna shule zaidi ya 108 lakini wameipa shule ya Puma.

Alisema madawati 66 yaliyosalia kutengenezwa kati ya hayo 71 ambayo yapo tayari halmashauri hiyo itatoa mbao 20 ili kuyatengeneza ambapo alitoa mwito kwa wananchi hao kuendeleza jitihada hizo za shughuli za maendeleo katika kata hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527