DAWA ZA CORONA ZAUZWA KWA MAGENDO KWA BEI YA JUU | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 8, 2020

DAWA ZA CORONA ZAUZWA KWA MAGENDO KWA BEI YA JUU

  Malunde       Wednesday, July 8, 2020

Uchunguzi wa BBC umebaini kuwa aina mbili za dawa ambazo zilitumika kutibu wagonjwa wa corona nchini India - remdesivir na tocilizumab - zimekuwa zikiuzwa katika soko la magendo kwa bei ya juu ndiyo maana kuna upungufu mkubwa sana wa dawa hizo.

Mwandishi wa BBC, Pandey anaripoti kutoka mji mkuu wa India Delhi.
Mjomba wake Abhinav Sharma alikuwa na homa kali na alikuwa anapata tabu kupumua wakati alipolazwa hospitalini huko Delhi.

Alikutwa na virusi vya corona na madaktari waliiambia familia yake itafute dawa aina ya remdesivir - dawa ambayo imeruhusiwa kwa ajili ya matibabu ya corona wakati wa dharura nchini India ",hii ikiwa ina maana kuwa madaktari wanaweza kutoa ruhusa ya matumizi ya dawa hizo kwa kutokana na sababu maalum.

Lakini upatikanaji wa dawa hiyo umeonekana kuwa jambo ambalo haliwezekani - dawa ya 'remdesivir' imeadimika na haipatikani kokote.

Bwana Sharma alihangaika kuwapigia watu kumsaidia kupata dawa ya kumsaidia mjomba wake ambaye hali yake ilikuwa inazidi kuwa mbaya kila saa.

"Nilikuwa na machozi machoni mwangu. Mjomba wangu alikuwa anapambana na maisha yake na nilikuwa nahangaika kupata dawa ambayo ingeweza kuokoa maisha yake," alisema.

"Baada ya kupiga simu kadhaa, nililipa mara saba ya gharama halisi ya dawa nilikuwa radhi kulipia gharama yoyote ile kwa kweli, lakini nawaonea huruma watu wale ambao hawana uwezo wa kununua kwa gharama hiyo," alisema.

Changamoto aliyokabiliana nayo Bwana Sharma, inazikabili familia nyingi sana mjini Delhi, ambapo watu wengi huwa wanahangaika na kufanya lolote ili kuokoa maisha ya wapendwa wao.

Baadhi wanasema huwa wanalazimika kulipa gharama kubwa sana kwa ajili ya dawa hiyo - wengi huwa wanaishia kwenye soko la zamani la dawa la mjini Delhi.

Via BBC SWAHILI
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post