ALIYEWAHI KUWA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI, JOSHUA NASSARI AHAMIA CCM | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 8, 2020

ALIYEWAHI KUWA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI, JOSHUA NASSARI AHAMIA CCM

  Malunde       Wednesday, July 8, 2020

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amejiunga Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza katika mkutano wa kupokelewa na viongozi wa CCM Mkoa wa Arusha Nassari amesema kuwa amejiunga chama hicho ili kujiweka katika upande mmoja na wale wanaoitakia nchi hii maendeleo.

Nassari ameongeza kuwa serikali ya Rais John Magufuli imefanya mambo mengi ambayo amekuwa akiyapigania kama vile kuboresha elimu, huduma za afya na ujenzi wa miundombinu pamoja na kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati, hivyo hakuna sababu yeyote ya kumpinga.

Nassari alivuliwa ubunge wake Machi 2019 kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya bunge mfululizo bila ruhusa, kitendo ambacho ni kinyume na sheria


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post