AJALI MBAYA YA LORI NA NOAH YAUA WATANO DODOMA


Watu 5 wamefariki  na 2 kujeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Noah lililokuwa likitokea Morogoro kwenda Dodoma kugongana na lori eneo la Kibaigwa jijini Dodoma.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amethibitisha.

Amesema ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva wa lori ambaye aliingia katikati ya barabara akitokea kwenye kituo cha mafuta bila kuangalia pande zote za barabara na kusababisha Noah kuingia uvunguni mwa lori.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527