RAIS WA UTPC DEOGRATIAS NSOKOLO ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA NSIMBO


Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratias Nsokolo leo Julai 16,2020 amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge katika Jimbo la Ndimbo mkoani Katavi.

Nsokolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabua ya Waandishi wa Habari mkoa wa Kigoma amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Nsimbo katika ofisi za CCM wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi

Nsokolo amesema amechukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge ili kutimiza haki yake ya kikatiba na  ili kama atapata nafasi ya kuchakuliwa aweze kuutumikia umma.

Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania Deogratias Nsokolo leo Julai 16,2020 akionesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge katika Jimbo la Ndimbo mkoani Katavi.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527