MAVUNDE AIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM JIMBO LA DODOMA MJINI

Anthony Mavunde
Na Alex Sonna,Dodoma
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde aibuka kidedea kwa kupata kura 904 katika kura za maoni za wagombea Ubunge CCM Jimbo la Dodoma Mjini.

Katika uchaguzi huo Mussa Adrew amepata kura 111, Robert Job 29 na Tadei Mwanga amepata kura 26.
Aidha jumla ya kura zilizopigwa ni kura 1189 na kura moja imeharibika na hivyo kula harari ni kura 1189.
Mavunde amewashukuru wajumbe kwa kura walizompa na kuwapongeza wagombea wezake kwa kushiriki katika uchaguzi huo.
“Hivyo naomba mniombee ili niweze kuteuliwa kuweza kuongoza bendera ya CCM Jimbo la Dodoma Mjini ili niendelee kuwatumikia kama mlivyokuwa mmenituma awali basi nikakamilishe yaliyosalia katika kuwaletea maendeleo wana Dodoma..

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post