RIDHIWAN KIKWETE AREJESHA FOMU YA UBUNGE CCM-CHALINZE | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, July 16, 2020

RIDHIWAN KIKWETE AREJESHA FOMU YA UBUNGE CCM-CHALINZE

  Malunde       Thursday, July 16, 2020
Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete leo Julai 16,2020 akikabidhi fomu kwa Katibu wa CCM Wilaya,Bi. Getrude Siyinza.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete akipitia fomu za kutia nia kiti cha Ubunge jimbo la Chalinze kabla ya kukabidhi  leo Julai 16,2020.

Na Andrew Chale - Chalinze
Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete leo 16 Julai, amerejesha fomu ya kuomba ridhaa kutetea tena kiti cha Ubunge wa jimbo hilo la Chalinze kwa kipindi chengine cha Miaka Mitano.

Ridhiwani amekabidhi fomu hizo leo kwa Katibu wa CCM Wilaya Bi. Getrude Siyinza. Hata hivyo hakuwa tayari kuzungumza lolote zaidi akiwaomba Wanachalinze kumuombea na kusubiria hatua inayofuata ya mchakato ndani ya chama.

"Nimerejesha fomu za kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Tupo pamoja na tuendelee kushirikiana na kuijenga CCM yetu na kuipa ushindi wa kishindo kwenye kura za Rais, Wabunge na Madiwani",alisema Ridhiwani Kikwete.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post