DR HUSSEIN MWINYI AJITOSA KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa katika serikali ya awamu ya Tano Dkt.Hussein Mwinyi achukua fomu kwa lengo la kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar katika ofisi za chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja Leo

Mara baada ya kukabidhiwa fomu, alikwenda eneo lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari.

Dk. Mwinyi ambaye ni Mbunge wa Kwahani visiwani Zanzibar amesema, “leo sikuja kuzungumza na waandishi wa habari, nimekuja kuchukua fomu tu na wala sina la kuzungumza.”

Amesema, hajajua kilichomo kwenye hizo fomu, hivyo akaomba aende akazisome kwanza ajue kilichomo.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527