WATANZANIA 57 WAREJEA KUTOKA AFRIKA KUSINI NA 38 KUTOKA MISRI


Watanzania 57 waliokuwa wamekwama nchini Afrika Kusini kutokana na janga la virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19 baada ya nchi hiyo kufunga mipaka yake hatimae wamerejea nyumbani.


Watanzania hao 57 waliokuwa wamekwama Nchini Afrika Kusini kwa takribani miezi mitatu baada ya uwepo wa zuio la kutoka nje (lockdown) wameondoka nchini humo kwa kutumia Shirika la ndege la Precission air kutokana na uratibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuhusisha Ubalozi wa Tanzania Nchini humo.

Wakizungumza kwa furaha katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo uliopo Afrika Kusini mmoja wa Watanzania hao aliyefahamika kwa jina la Sunderland the only one ameishukuru Serikali kupitia kwa Balozi wa Tanzania nchini humo Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi kwa kuwa pamoja nao katika kipindi chote ambacho wamekuwa katika zuio Afrika Kusini.

Kundi jingine kama hilo la watanzania 38 waliokuwa wamekwama Nchini Misri nao wamefanikiwa kuondoka nchini humo kwa shirika la ndege la fly Egypt.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527