TAKUKURU YAANZA RASMI KUWAHOJI WABUNGE 69 WA CHADEMA

Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

Taasisi ya kuzuia na kupambana  na rushwa  nchini TAKUKURU imeanza rasmi  kuwahoji  Wabunge  69 wa Chama cha Demokrasia  na Maendeleo (CHADEMA) jijini  Dodoma  ambapo jana  baadhi ya Wabunge wa Chama hicho waliitikia wito kwa kufika katika Ofisi hizo kuhojiwa.

Wabunge ambao tayari wameshafika katika Ofisi hizo ni pamoja na Joseph Mbilinyi almaarufu Sugu Mbunge wa Mbeya Mjini,Peter Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Lijualikali Mbunge wa Kilombero, Halima Mdee Mbunge wa Kawe pamoja na Esther Bulaya Mbunge wa Bunda Mjini.

Aliyekuwa wa kwanza kufika katika viwanja vya Takukuru ni Joseph Mbilinyi Mbunge  wa Mbeya Mjini ambaye alifika saa1 na dakika 55 asubuhi na kuhojiwa kwa takriban  saa2 ambapo alitoka saa4 asubuhi.

Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali  alifika saa2.20asubuhi huku peter Msigwa ambaye ni Mbunge wa Iringa Mjini akifika katika Ofisi hizo  saa nne na robo asubuhi.

Mbunge wa Momba mkoani Songwe David Silinde aliwasili TAKUKURU Makao Makuu majira ya saa tano na dakika 41 asubuhi.

Akizungumza nje ya viwanda vya Takukuru mara baada ya kuhojiwa Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali alisema kuwa Mahojiano yalikuwa yakirafiki kabisa huku akuwataka Wabunge wenzake watakaohojiwa kuwa wakweli kutokana na Taasisi hiyo kujipanga na inafahamu kila kitu.

Wabunge hao  wa CHADEMA wamefika kwa nyakati tofauti  katika Ofisi hizo za TAKUKURU Makao Makuu kuhojiwa  ikiwa ni mwendelezo wa uchunguzi unaoendeshwa na TAKUKURU Makao makuu wa malalamiko dhidi ya matumizi  ya fedha za CHADEMA ambapo hatua iliyopo sasa ni ya kuwahoji Wabunge 69 Wanachama na waliowahi kuwa wanachama wa Chama hicho.

Fedha hizo ni zile ambazo zilililalamikiwa na waliokuwa Wabunge wa Chadema ambao walitangaza kukihama Chama chao na katika malalamiko yao walidai kwamba walikuwa wakikatwa fedha katika mishahara yao kila mwezi kuanzia mwezi Juni 2016  ambapo Kwa mujibu wa malalamiko hayo kila mwezi,Wabunge wa Viti Maalum walikuwa wakikatwa kiasi Sh Milioni 1 laki5 na 60elfu ambapo Wabunge wakuchaguliwa kwenye Majimbo walikuwa wakikatwa Sh 520,000 na kwamba hawakuwa wakifahamu namna ambavyo fedha hizo zimeekuwa zikitumika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527