SERIKALI YATOA MUDA WA MPITO KUWANUSURU WAFANYABIASHARA WA MADINI NCHINI

Waziri wa Madini Dotto Biteko

Wizara ya madini imetoa muda wa mpito wa miezi mitatu kwa wafanyabiashara na wasafirishaji wa madini nchini kununua madini popote katika kipindi hiki cha ugonjwa wa corona ili kuhakikisha soko la madini halitetereki huku ikiwaonya wafanyabisha hao kutotumia mwanya huo kutorosha madini pamoja na kukwepa kodi.


Agizo hilo limetolewa na waziri wa madini Dotto Biteko Mkoani Geita wakati akizungumza na wafanyabishara na wasafirishaji wa madini akibainisha kuwa serikali imetoa unafuu huo ili kuwasaidia wafanyabiashara kutoyumba kiuchumi katika kipindi hiki cha janga la Covid 19. 

Waziri Biteko amesema wizara ya madini inatarajia kukusanya bilioni mia tano kwa mwaka huu kutoka kwenye mrabaha wa madini kutokana na kuvuka lengo la kukusanya zaidi ya bilioni mia nne mpaka sasa.

Mwenyekiti wa Halmashuri ya mji wa Geita Leonard Bugomora amesena mkoa wa Geita umenufaika na fedha kutoka migodi mikubwa ukiwemo GGM ambapo wameweza kujenga kituo cha uwekezaji,uwanja wa mpira pamoja na masoko ya wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post