RATIBA LIGI KUU KUANZA NA VIPORO JUNI 13


Ligi Kuu Tanzania Bara itarejea kwa kuanza na mechi za viporo kwa timu zilizocheza mechi pungufu huku ikipangwa kumalizika Julai 27 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu Juni 1, Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo amesema wameona bora wamalizane na viporo kisha Ligi ndio iendelee kama kawaida.

“Tarehe 13 ambapo Ligi inarudi kutakuwa na mchezo na tarehe 14 pia kutakuwa na mchezo tarehe 20, hizi mechi zote ni viporo tukimaliza ndio tutaendelea na Ligi,”.

Akizungumzia namna Ligi itakavyochezwa na kumalizika lini, Kasongo alisema watatoa ratiba kamili kwa klabu pamoja na vyombo vya habari vyote.

“Ligi itaendelea tarehe 20 Juni hapo baada ya kumaliza viporo vyetu na tunatarajia imalizike tarehe 27 Julai mwaka huu,” alisema Kasongo

Kwa upande wa timu zitakazopanda na kushuka, alisema wameweka utaratibu wa kuchezwa mechi za mchujo (Play Off) kuanzia tarehe 29 mwezi wa saba ikiwa ni siku mbili tu baada ya Ligi Kuu kumalizika, mechi zamarudiano zikichezwa Agosti Mosi na baada ya hapo ndio atajulikana yupi atashuka na nani atapanda.

Akizungumzia upande wa Ligi daraja la kwanza, Kasongo alisema Ligi hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi tarehe 19 mwezi wa sita mpaka tarehe 12 mwezi wa saba.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527