RAIS SHEIN AIVUNJA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR


Rais wa Serikali za Mapinduzi Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein  leo Jumamosi tarehe 20 Juni 2020 amelivunja Baraza la Wawawakilishi la Zanzibar.

Akizungumza wakati anavunja baraza hilo, Rais Shein amepongeza uongozi wa baraza hilo kwa kazi nzuri uliyoifanya, kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Zanzibar.

Rais Shein amesema katika kipindi cha miaka mitano, baraza hilo limefanya kazi kubwa ya kuwatumikia wananchi, ikiwemo kupitisha bajeti za serikali na kutunga sheria mbalimbali.

Rais Shein anamalizia kipindi chake cha mihula miwili ya uongozi (2010/2015 na 2015/2020).Makada mbalimbali wameanza kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea urais wa Zanzibar kupitia CCM


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527