KAMATI YA UTEKELEZAJI YA UVCCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI YAFANYA ZIARA KUKAGUA UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU


Kamati ya utekelezaji ya UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatatu Juni 15,2020 imefanya ziara kuona maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya Comrade Dotto Joshua na Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Agnes Bashemu (Mtoto wa Mama).

Wajumbe kwa pamoja wamepongeza na maendeleo ya Ujenzi ambapo Ujenzi umefikia hatua nzuri ya ukamilishaji wa Boma la nyumba.

Kamati ya Utekelezaji kwa kauli moja, imetoa  shukrani kwa wadau wote ambao wamekuwa bega kwa bega katika kuhakikisha Ujenzi unakamilika na kwamba Kamati inaendelea kuwaomba wadau Mbalimbali kuendelea kujitoa kwa moyo wa hali na mali ili kufanikisha Ujenzi wa Nyumba ya katibu UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini.

Sambamba na hivyo, Kamati ya utekelezaji imetoa pongezi za Dhati kwa Mwenyekiti UVCCM Taifa Comrade Kheri Denice James (MCC) Pamoja na Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa kwa Maono yao ya Kuhakikisha watendaji wa Jumuiya ya Umoja wa CCM wanakuwa na Makazi Bora na Uhakika

Imetolewa na Idara Ya Hamasa &Chipukizi

Peter Mgalula
Kamati ya utekelezaji ya UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakishiriki  ujenzi wa nyumba ya katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527