HALMASHAURI YAPEWA JUKUMU UKAMILISHAJI MIRADI MAENDELEO



Madiwani wa manispaa ya Shinyanga wameutaka uongozi wa manispaa hiyo kukamilisha miradi yote ya maendeleo, ambayo haijakamilika iliyoanzishwa ndani ya miaka mitano na madiwani hao ili ikamilike na kuanza kutoa huduma kwa jamii.


Hayo yamebainishwa leo Juni 9, 2020 kwenye Baraza maalumu la madiwani wa manispaa hiyo ambalo ni la mwisho, kuwa kuna miradi mingi ya maendeleo ambayo ilianzishwa kipindi cha utawala wa madiwani hao tangu mwaka 2015, ambayo mingine bado haijamalizika kujengwa.

Baadhi ya Madiwani hao akiwemo David Nkulila wa Ndembezi, walisema ndani ya utawala wao wa miaka mitano, kuna miradi mingi ya maendeleo ambayo wameianzisha, ikiwamo ya ujenzi wa maboma ya zahanati, madarasa, mabweni, vyoo vya shule, bararaba, machinjio, dampo, ambapo mengine haijakamilika.

“Sisi madiwani tunamaliza muda wetu wa kutumikia wananchi katika manispaa hii ya Shinyanga, lakini kuna miradi ya maendeleo ambayo tuliianzisha ndani ya utawala wetu wa miaka mitano tangu 2015, ambapo mingine haijakamilika kujengwa, hivyo jukumu hili tunaliacha kwa menejimenti ya manispaa kuikamilisha,” walisema madiwani kwa nyakati tofauti

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alisisitiza uongozi huo wa manispaa ya Shinyanga, wazungukie miradi yote ya maendeleo iliyotekelezwa na kuibaini ile ambayo haijakamilika, ili wapate kutengewa fedha kupitia makusanyo ya ndani na kuikamilisha haraka.

Katika hatua nyingine Mboneko aliwataka madiwani watakaorudi kugombea, wakafanye siasa za kistaarabu, ikiwa Serikali imejipanga vyema kuhakikisha uchaguzi huo mkuu utafanyika kwa amani na utulivu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Magulumbi, alisema maelekezo yote yaliyotolewa watayafanyia kazi, kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya manispaa hiyo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye baraza la madiwani wa Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele, akizungumza kwenye baraza hilo.

Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Mkadam akizungumza kwenye kikao cha baraza hilo.

Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga John Peter Kisandu, akizungumza kwenye kikao cha baraza hilo la madiwani.


Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akizungumza kwenye baraza hilo na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa.

Madiwani wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza lao la mwisho.

Diwani wa vitimaalum Mariam Nyangaka, akizungumza kwenye baraza hilo.

Diwani wa Ngokolo Emmanuel Ntobi, akizungumza kwenye baraza hilo.

Diwani wa Ndembezi David Nkulila, akizungumza kwenye baraza hilo.

Diwani wa Ndala, Wiliamu Shayo akizungumza kwenye baraza.

Watendaji wa kata manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani wakifuatilia baraza hilo.

Watendaji wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani wakifuatilia baraza hilo.

Picha zote na Marco Maduhu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527