MCHUNGAJI MSIGWA ATANGAZA RASMI NIA TA KUGOMBEA URAIS 2020


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mbunge wa Iringa Mjini ,Mchungaji Peter Msigwa ametangaza Rasmi kuwania Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu.Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma Mchungaji Msigwa amesema amesema kwa mujibu wa kanuni na Taratibu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA]tayari ameshawasilisha ombi la kuomba kuwania kinyang’anyiro hicho.


Mchungaji Msigwa amesema ameamua kuwa na nia kuwania kugombea Urais ili aweze kuleta maendeleo.


“Kwa  mujibu wa taratibu ya Chama chetu nimeamua kuomba ridhaa ya kuwania Urais na lengo hasa ni kuleta maendeleo makubwa na si madogodogo ,na nitajitahidi kuleta Maendeleo ya kweli kwani nchi yetu ina rasimali nyingi sana    na tumeachwa nyuma sana kimaendeleo”amesema Msigwa.

Kuhusu jimbo lake la Iringa Mjini,Mchungaji Msigwa amesema iwapo chama chake hakitampitisha kugombea Urais ataendelea kulitetea jimbo la Iringa Mjini.

“Kwa Vile leo nimetangaza rasmi kuwania Urais isije watu wakafikiri kuanza kujisogeza kugombea Ubunge katika jimbo langu la Iringa Mjini, bado ni mapema sana hivyo iwapo chama changu hakitanipitisha nitaendelea kutetea kiti change cha ubunge kwa miaka mingine mitano ijayo hivyo wale wanaotamani jimbo langu la Iringa Mjini waombee nipitishwe na Chama lakini nisipopitishwa nitagombea ubunge kupitia chama Changu na nitamtetea kwa nguvu zote mgombea Urais atakayepitishwa  iwapo mimi nitashindwa kwa sababu lengo ni moja tu kuing’oa  CCM madarakani”amesema Mchungaji Msigwa.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527