MBUNGE WA NKASI CCM, ALLY KESSY ATAKA RAIS MAGUFULI AONGEZEWE MUDA....SPIKA NDUGAI AMJIBU | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, June 10, 2020

MBUNGE WA NKASI CCM, ALLY KESSY ATAKA RAIS MAGUFULI AONGEZEWE MUDA....SPIKA NDUGAI AMJIBU

  Malunde       Wednesday, June 10, 2020

Mbunge wa Nkasi CCM, Ally Kessy ameliomba Bunge kumuongezea muda wa kutawala Rais John Magufuli hata kama yeye Rais hataki kwa kubadili Ibara inayoweka kikomo cha kipindi cha urais.

Akijibu hoja hiyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtaka Kessy kuileta hoja hiyo baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu katika Bunge la 12 ambapo ameahidi kulishughulikia.

“Mheshimiwa Keissy ngoja tuende uchaguzi mkuu, turudi, na mimi naamini sote tunarudi. Hilo ulishikie uwe nalo moyoni, tutarudi hapa [bungeni] salama, azimio hilo utakuja kulileta wewe Mzee Keissy na litapita kwa kishindo, atake asitake [Rais Magufuli] tutaongeza muda,”  Amesema  Spika Job Ndugai

Itakumbukwa kuwa Rais Magufuli amekwisha kataa hadharani wazo la kuongeza muda wa kuongoza nchi.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post