MTOTO WA MIAKA 4 AUAWA KWA KUKATWA PANGA SHINYANGA...MUUAJI NAYE AUAWA

Picha haihusiani na habari hapa chini

Na mwandishi wetu- Shinyanga Press Club blog
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la James Mhoja(36)ameuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumuua mtoto wa dada yake mtoto Emmanuel John(4) kwa kumkata mapanga wakati akicheza na watoto wenzake nyumbani kwao.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Joseph Paul amesema tukio hilo lilitokea jana Juni 9 majira ya saa 9 alasiri kwenye Mtaa wa Ndala Manispaa ya Shinyanga, wakati mtoto huyo alipokuwa anacheza nje ya nyumba yao ndipo mtu huyo alimvamia na kumshika kisha kuanza kumkata mapanga.

"Mtuhumiwa wa mauaji ya mtoto huyo naye aliuawa na wananchi kwa kumponda mawe na katika uchunguzi wetu wa awali,tumebaini alikuwa anatatizo la ugonjwa wa akili na bado tunaendelea na uchunguzi wa tukio hili"amesema kaimu Kamanda Paul.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527