Picha : MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AZINDUA RASMI MRADI WA MAJI UZOGORE


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amezindua Rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga uliojengwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) na wananchi ukigharimu jumla ya shilingi milioni 88.8.

Akizungumza wakati wa kuzindua Mradi huo leo Alhamis Juni 18,2020, Mboneko amewataka wananchi wa Uzogore kutunza miundo mbinu ya maji ili iweze kudumu kwa kipindi kirefu na kuwasisitiza viongozi wa eneo hilo wasimamie wananchi wapate huduma ya maji muda wote.

“Wananchi wa kijiji hiki wakiongozwa na Mwenyekiti wa kijiji walikuja ofisini kwangu wakileta kilio cha Wana Uzogore,nami nikaamua kuja mwenyewe Uzogore kuwasikiliza Septemba 16,2019 kutokana na kwamba serikali ni sikivu na inatekeleza yale wananchi wanayataka. Niwapongeze SHUWASA na RUWASA ambao nao baada ya kuwaambia kuwa wananchi wanahitaji maji wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mnapata maji na leo mnaanza kupata huduma ya maji safi na salama”,alisema Mboneko.

“Kufanikiwa kwa mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2015 ya kumtua ndoo mwanamke kichwani na kumpunguzia umbali mrefu kutafuta maji”,alisema Mboneko.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa wilaya alisema baada ya maji kufika Uzogore sasa awamu inayofuata na kufikisha maji katika kijiji cha Bugwandege.

Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Emael Nkopi alisema ujenzi wa mradi wa Maji Uzogore ulioanza Februari 5,2020 na kukamilika Juni 5,2020 ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa wanakijiji wa Uzogore uliofanyika Septemba 16,2019 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

Alisema Katika mkutano huo uliojadili namna ya kuwapatia wananchi huduma ya maji safi na salama,wananchi walikubaliana kutoa maeneo yao bila gharama yoyote katika njia za bomba na sehemu ya kujenga vituo (DP) ya magati ya kuchotea maji pamoja na kujitolea nguvu kazi katika uchimbaji wa mitaro ya kupitisha bomba.

“Gharama halisi zilizotumika katika ujenzi wa mradi wa Maji katika Kijiji cha Uzogore utakaonufaisha wakazi 3,778 ni shilingi 88,830,000/= ambapo kati ya hizo, RUWASA wilaya ya Shinyanga imetoa shilingi 50,400,000/=, SHUWASA shilingi 31,690,000/= na nguvu kazi ya wananchi (kuchimba mitaro na kufukia) shilingi 6,740,000/=”,alieleza.

“Katika utekelezaji wa mradi wa kusambaza maji ya bomba katika kijiji cha Uzogore jumla ya mita 6720 za mtandao wa mabomba zimelazwa,Stand Pipe mbili katika taasisi za umma (shule ya msingi Uzogore 1 na shule ya sekondari Uzogore 1) na vituo vya kuchotea maji/maghati matano yamejengwa katika vitongoji vya Uzogore Centre,Majengo A,Majengo B,Shimarulwe na Ikulilo”,alieleza Nkopi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa SHUWASA, Bi. Flaviana Kifizi alisema SHUWASA kwa kushirikiana na RUWASA walitoa hadi ya kupeleka maji Uzogore na wametekeleza ili kumtua mwanamke ndoo kichwani.

“Kazi ya RUWASA ni kujenga miundo mbinu ya maji kuelekea maeneo ambayo hajafikiwa na huduma ya maji,RUWASA wamemaliza kazi yao,tumejenga sehemu za kuchotea maji (vioski),tumeleta maji hapa kutoka Ziwa Victoria ili kumtua ndoo mwanamke kichwani. Tunaomba wananchi muunge maji majumbani mwenu kwa gharama zenu na tutawaungia maji ndani ya muda mfupi”,alisema Kifizi.

Nao wakazi wa Uzogore wameeleza kufurahia kuanza kupata huduma ya maji safi na salama na kuondokana na adha ya muda mrefu ya kusafiri umbali mrefu kufuata maji.


ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza leo Alhamis Juni 18,2020 wakati wa kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga uliojengwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) na wananchi ukigharimu jumla ya shilingi milioni 88.8. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Ibadakuli,Joseph Sengerema, kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Uzogore Peter Dotto. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza leo Alhamis Juni 18,2020 wakati wa kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga.
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Emael Nkopi akielezea kuhusu ujenzi wa mradi wa Maji Uzogore ulioanza Februari 5,2020 na kukamilika Juni 5,2020 na kugharimu jumla ya shilingi milioni 88.8.
Mkurugenzi wa SHUWASA, Bi. Flaviana Kifizi akizungumza wakati wa kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga uliojengwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) na wananchi.
Mkurugenzi wa SHUWASA, Bi. Flaviana Kifizi akiwahamasisha wananchi wa kijiji cha Uzogore kuunganisha huduma ya maji hadi majumbani mwao.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga uliojengwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) na wananchi ukigharimu jumla ya shilingi milioni 88.8.
Maandishi yakisomeka Mradi wa Maji ya Bomba Uzogore umezinduliwa rasmi na Mhe. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Ndg. Jasinta V. Mboneko tarehe 18 Juni 2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko na viongozi mbalimbali wa SHUWASA,RUWASA,Vyama vya Siasa na wananchi  wakifurahia wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga uliojengwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) na wananchi ukigharimu jumla ya shilingi milioni 88.8.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifungua bomba la maji katika kituo cha kuchotea maji kwenye Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifungua bomba la maji katika kituo cha kuchotea maji kwenye Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifungua bomba la maji katika kituo cha kuchotea maji kwenye Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore.  
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore.  
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifurahia jambo baada ya kumtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore.  
Wa tatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akizungumza baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akipiga picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na wananchi baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akipiga picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na wananchi baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akipiga picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na wananchi baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akipiga picha ya pamoja na wananchi baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akipiga picha ya pamoja na wananchi baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akipiga picha ya pamoja na  viongozi wa CCM baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akipiga picha ya kumbukumbu baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akipiga picha ya kumbukumbu baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akipiga picha ya kumbukumbu baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Uzogore Peter Dotto akizungumza wakati wa kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga uliojengwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) na wananchi.
 Mwenyekiti wa CCM kata ya Ibadakuli,Joseph Sengerema akizungumza wakati wa kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga uliojengwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) na wananchi.
Katibu waakizungumza wakati wa kuzindua rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga uliojengwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) na wananchi.
Wakazi wa Uzogore wakifuatilia zoezi la uzinduzi wa mradi wa maji.
Mkazi wa Uzogore Hamid Rashid akitoa shukrani kwa kupata mradi wa maji katika kijiji cha Uzogore.
Mkazi wa Uzogore aliyejulikana kwa jina moja la Nasra akitoa shukrani kwa kupata mradi wa maji katika kijiji cha Uzogore.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza na wachezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana Uzogore (waliovaa jezi nyekundu) na Veterani Uzogore baada ya kuzindua Rasmi Mradi wa Maji ya Bomba kijiji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga. Akiwa katika kijiji cha Uzogore Septemba 16,2019 kusikiliza kero za wananchi ikiwemo ya maji, Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba wakazi wa eneo waunde timu na leo wakati akizindua mradi wa maji timu hizo zimecheza mechi katika uwanja wa Uzogore huku Mkuu huyo wa wilaya akishuhudia mtanange huo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akisalimiana na wachezaji na kukagua Timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana Uzogore
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akisalimiana na wachezaji na kukagua Timu ya Mpira wa Miguu ya Veterans Uzogore.
Mchezo kati ya Vijana Uzogore na Veterans Uzogore ukiendelea ambapo Vijana Uzogore waliibuka washindi kwa kuwafunga Veterans Uzogore magoli 3-0.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko na viongozi mbalimbali wakifuatilia Mchezo kati ya Vijana Uzogore na Veterans Uzogore ambapo Vijana Uzogore waliibuka washindi kwa kuwafunga Veterans Uzogore magoli 3-0.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza baada ya Mchezo kati ya Vijana Uzogore na Veterans Uzogore kumalizika ambapo Vijana Uzogore waliibuka washindi kwa kuwafunga Veterans Uzogore magoli 3-0. Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuendelea kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi zawadi ya mbuzi mmoja kwa timu ya Veterans Uzogore. 
Wachezaji wa timu ya Veterans Uzogore wakifurahia zawadi ya mbuzi kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe, Jasinta Mboneko.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi zawadi ya mbuzi mmoja kwa timu ya Vijana Uzogore (wenye jezi nyekundu).
Wachezaji wa timu ya Vijana Uzogore wakifurahia zawadi ya mbuzi kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe, Jasinta Mboneko.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527