Picha: KANISLA KKKT LATOA VIFAA VYA KISASA KWA WAKUU WA MAJIMBO NA WACHUNGAJI KUENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA CORONAKanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, limetoa vifaa vya kisasa kwa wakuu wa majimbo na wachungaji wa kanisa hilo, kutoka Shinyanga na Simiyu  kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.


Zoezi la utoaji wa vifaa hivyo limefanyika leo Juni 23,2020 katika Kanisa la KKKT Mjini Shinyanga, na kuhudhuriwa na wakuu hao wa majimbo pamoja na wachungaji, huku pia ikiendeshwa ibada mfupi ya kuweka wakfu vifaa hivyo pamoja na kuliombea taifa kuondokana na virusi hivyo vya Corona.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala, amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, pamoja na kuzingatia maelekezo ya Serikali, kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, kuvaa barakoa, kupaka vitakasa mikono ili waendelee kuwa salama.

“Natoa wito kwa wananchi wasividharau virusi vya Corona, bali waendelee kuchukua tahadhari ya kujikinga pamoja na kufuata maelekezo ya Serikali, kwa kunawa mikono kwa sabuni na majitiririka, kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko ya watu wengi na kutokaa makundi,” amesema Askofu Makala.

Aidha amevitaja vifaa ambavyo wamevitoa kuwa ni Barakoa, Sabuni, pamoja na vifaa vya kisasa vya kunawia mikono kwa maji tirika bila ya kugusa koki ya maji wala sabuni, ambavyo vinatumika kwa kukanyaga kwa miguu, kwa kushirikina na kanisa la Kilutheri Bavaria la Ujerumani ili kuendelea kuchukua tahadhari zaidi,

Naye Mchungaji Patrick Zengo wa Usharika wa Kanani (KKKT) Ndembezi manispaa ya Shinyanga, akizungumza kwa niaba ya wenzake, ameshukuru msaada wa vifaa hivyo ambavyo vitawasaidia kuendeleza mapambano ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa waumini wao.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (Shinyanga na Simiyu), Dkt. Emmanuel Makala, akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya kukabiliana na Corona kwa wakuu wa majimbo na wachungaji wa kanisa hilo, kutoka Shinyanga na Simiyu leo Jumanne Juni 23,2020 - Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (Shinyanga na Simiyu), Dkt. Emmanuel Makala akinawa mikono wa sabuni na maji tiririka kabla ya kuanza kugawa vifaa hivyo, vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (Shinyanga na Simiyu), Dkt. Emmanuel Makala akiweka wakfu vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, kabla ya kuanza kuvigawa.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (Shinyanga na Simiyu), Dkt. Emmanuel Makala (kulia),akimkabidhi vifaa vya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona mchungaji Patric Zengo Usharika wa Kaanani Ndembezi kwa niaba ya wenzake,

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (Shinyanga na Simiyu), Dkt. Emmanuel Makala (kushoto),akimkabidhi vifaa vya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona mchungaji Patric Zengo Usharika wa Kaanani Ndembezi.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (Shinyanga na Simiyu), Dkt. Emmanuel Makala akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Zoezi la ugawaji vifaa vya kujikinga na virusi vya Corona likiendelea.

Zoezi la ugawaji vifaa vya kujikinga na virusi vya Corona likiendelea.

Muonekano wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka ili kuendeleza mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Wachungaji na wakuu wa majimbo wakiwa wamebeba barakoa kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kujikinga na virusi vya Corona.

Wachungaji na wakuu wa majimbo wakiwa wamebeba barakoa kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kujikinga na virusi vya Corona.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (Shinyanga na Simiyu), Dkt. Emmanuel Makala, katikati mwenye vazi jeupe, akipiga picha ya pamoja na wakuu wa majimbo na wachungaji, mara baada ya kumaliza kuwakabidhi vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527