KIJANA AMUUA BABA YAKE KWA KUMTWANGA NGUMI USONI MOROGORONa Mwandishi wa Malunde 1 blog - Morogoro
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Yohana Isaya Lameck (17) mkazi wa Kitongoji cha kata ya Mkalama Manyani wilayani Gairo kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Isaya Lameck (41) kwa kumpiga ngumi usoni na kumkanyaga sehemu mbalimbali za mwili.

 Kamanda wa polisi mkoa wa wa Morogoro SACP Wilbroad Mutafunga amesema tukio hilo limetokea Mei 31,2020 majira ya saa 12 alfajiri.

"Isaya Lameck aliuawa kwa kupigwa ngumi usoni na kukanyagwa sehemu mbalimbali za mwili wake na mtoto wake wa kumzaa Yohana Isaya",amesema.

"Kabla ya tukio hilo marehemu alirudi nyumbani kwake akiwa katika hali ya ulevi,ndipo ulipozuka ugomvi kati yake na mtoto ambaye alimpiga baba yake kwa ngumi usoni na kudondoka chini kisha kuendelea kumkanyaga sehemu za tumboni hali iliyosababisha baba huyo kupata maumivu makali katika mwili wake",amesema Kamanda Mutafugwa.

Amesema utokana na ugomvi huo,ndugu waliamua kuamua ugomvi huo na kumpatia matibabu na alfajiri ya Mei 31,2020 aligundulika kuwa amefariki dunia na mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi. 

Amesema mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527