JAMAA ANUSURIKA KUFA BAADA KUFYEKA SEHEMU ZAKE ZA SIRI 'MAKENDE' KWA KISU SHINYANGA

Picha haihusiani na habari hapa chini

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katika hali isiyokuwa ya kawaidia mwanaume aliyejulikana kwa jina la Malembeka Jisinza (50) mkazi wa kijiji cha Bugimbagu kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga amenusurika kufa baada ya kujikata sehemu zake za siri kende' zote mbili kwa kutumia kisu.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul tukio hilo limetokea Juni 22,2020 majira ya saa 12 na jioni katika kijiji cha Bugimbagu kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.

“Jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa tukio la kujaribu kujiua ambapo siku ya tukio Malembeka Jisinza mkazi wa Bugimbagu akiwa nyumbani kwake alijikata sehemu za siri (kende) zote mbili kwa kutumia kisu na pia alijikata sehemu ya tumbo juu ya kitovu”,amesema Kamanda Paul.

Amesema chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa na mtuhumiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na kwamba hali yake siyo nzuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527