WANACHAMA 11 WA CHADEMA WAJITOKEZA KUGOMBEA URAIS TANZANIA 2020


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo Juni 17, 2020, kimetangaza majina ya Wanachama wake 11 walioomba kuteuliwa na Chama hicho kugombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba.

Majina hayo yametajwa leo ambapo imesisitizwa kuwa mchakato wa awali ulikuwa unahusisha kuandika barua ya kitia nia na sio kuchukua na kurudisha fomu, hivyo watu walioandika barua kwa Katibu Mkuu John Mnyika ni 11.

Wanachama hao wametajwa akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu na Peter Msigwa.

Wengine ni kada wa zamani wa CCM na mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu, Mwita Isaya, Dkt Majinge Mayrose, Manyama Leonard, Nicodemus Gasper, Nalo Opio, Neo Richmond na Shaaban Msafiri.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa kuna baadhi ya wanachama ambao wameelezwa kuwa ni bodaboda walijikusanya na kumwandikia barua mtu mmoja (ambaye hajatajwa) ili agombee lakini barua yao haikukidhi vigezo kutonana na kuwepo kwa sharti la mtu mwenyewe kuandika barua na sio kuandikiwa.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527