IMF YAISAMEHE TANZANIA DENI LA MABILIONI YA PESA


Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) imeidhinisha msamaha wa madeni ya Serikali ya Tanzania wa  Dola za Marekani 14.3 milioni inayodaiwa na shirika hilo ili zisadie katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Fedha hizo zilitakiwa kulipwa na Tanzania kwa IMF ikiwa ni sehemu ya malipo ya madeni inayodaiwa.

Taarifa ya IMF ya Juni 10, 2020 imesema msamaha huo wa sawa na Sh33.1 bilioni ni wa miezi minne hadi Oktoba 13, 2020 ambapo Tanzania haitalipa malipo ya madeni ya mkopo wake yenye thamani ya kiwango hicho inachodaiwa na shirika hilo.

IMF imesema janga la Corona limeathiri uchumi wa Tanzania hasa katika shughuli za utalii na kasi yake inaweza kuendelea kushuka zaidi, hivyo msamaha huo utasaidia kupunguza athari hizo.

Akizungumzia msamaha huo, Rais John Magufuli ameishukuru IMF  kwa kutambua hatua za Serikali ilizochukua katika mapambano ya Corona na kuipatia Tanzania ahueni ya malipo ya madeni.



“Leo ninapozungumza tumepata fedha za masamaha, bodi ya wakurugenzi IMF imeidhinisha leo dola 14.3 milioni za msamaha wa kodi ya madeni tuliyokuwa nayo, na kwa sababu tulipambana vizuri sana na ugonjwa wa corona, msamaha huo umekuja wakati muafaka,” amesema Rais Magufuli.

Amesema kwa sasa Corona imepungua sana lakini Watanzania wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post